Gladness Mallya na Erick Evarist, Dar es SalaamULE uchumba uliodumu kwa muda mrefu kati ya mastaa filamu na muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamis Baba ‘H. Baba’ na Flora Mvungi umefikia pazuri baada ya H – Baba kumtolea mahari na kumvalisha pete ya uchumba.
H-Baba akimvisha pete ya uchumba, Flora Mvungi.ONA TOFAUTI
Kinyume na ilivyozoeleka, zoezi la kutoa mahari kufanyika nyumbani, kwa wawili hawa ilikuwa tofauti kwani kila kitu kilimalizikia ukumbini humo.
H-Baba akiwasalimiana ndugu na jamaa.
Flora Mvungi kabla ya kuvishwa pete ya uchumba.“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila kuomba mchango kwa mtu yoyote.
“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi wangu.”
MASTAA
Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Hisani Muya ‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).
Ndugu na jamaa waliohudhuria tukio hilo.
H-Baba na mchumba wake Flora Mvungi wakiwa na msanii Dude (kulia).
H-Baba akiwasalimia wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment