EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 31, 2012

Kova kuanza kusaka mtandao wa vipeperushi.

Waandishi Wetu
POLISI nchini wamepanga kusambaratisha mtandao unaodhamini na kuchapisha vipeperushi vinavyohamasisha kufanyika kwa maandamano, kutaka kutolewa kwa Katibu wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda  Issa Ponda na wenzake.Hatua hiyo imekuja baada ya waumini hao kupanga kufanya maandamano  Novemba Mosi, ambayo yatahamasisha mahakama hiyo kutoa dhamana kwa kiongozi wa taasisi hiyo na wenzake.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema wataanza kufanya msako wa wote wanaohamasisha, wanaochapisha na wanaotoa vipeperushi ili kuwakamata.
“Tunafuatilia wadhamini na wachapishaji wa vipeperushi kwani ni chanzo cha uchochezi na upotevu wa amani nchini,” alisema Kova.Kova alisema maandamano hayo ambayo yamepangwa na waumini hao yanatishia amani , wananchi watashindwa kwenda kazini na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
“Hatuna mazungumzo tena kwa suala lolote litakalotishia uvunjifu wa amani hasa kwa yeyote atakayefanya maandamano bila kibali, hatutangalia anatoka dini gani au chama gani hivyo polisi itafanya kazi yake na kuwachukulia hatua kali,” alisema Kova na kuongeza:“Kisheria kumtishia mtu siyo lazima utumie bomu, bali unaweza ukatumia kauli au vipeperushi kama hivyo vya maandamano.”Alisema wazazi watakaoruhusu watoto wa shule kufanya maandamano watachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani, ikiwezekana  kufungwa mwaka mmoja jela.“Nimesikia wanataka kuwahusisha watoto wasiende shule, ili wafanye maandamano ambayo yanazuiwa na sheria ya mtoto kutofanya maandamano,” alisema Kova na kuongeza:
 
“Sisi tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake, kama kuna mtu amefikishwa mahakamani kuna taratibu zake za kupata dhamana, siyo kufanya maandamano haramu.”
Pia, aliwaomba wananchi wasishiriki maandamano hayo kwani yataleta madhara makubwa kwa familia zao kwa wale watakaokamatwa.“Hii inajidhihirisha pale utakapotembelea familia za wale waliokamatwa katika maandamano yaliyopita, watoto wanashindwa hata kwenda shule kutokana na kukamatwa kwa wazazi wao na wanakosa nauli na chakula,” alisema Kamanda Kova.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate