AZOZANA NA SHYROSE, NUSURA WAZIPIGE UKUMBINI KABLA YA UCHAGUZI
Habel Chidawali, Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ameendeleza ubabe wake dhidi ya hasimu wake kisiasa, Anne Kilango baada ya kumbwaga kwa idadi kubwa ya kura katika uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).
Habel Chidawali, Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ameendeleza ubabe wake dhidi ya hasimu wake kisiasa, Anne Kilango baada ya kumbwaga kwa idadi kubwa ya kura katika uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).

Hii
ni mara ya pili kwa Simba kumshinda Kilango katika kuwania nafasi ya
uenyekiti wa UWT, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2008, ambapo Simba
aliibuka mshindi.
Katika uchaguzi huo uliofanyika mjini Dodoma
ukisimamiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Tibaijuka, Sophia Simba alipata kura….. huku Kilango akipata kura
…. na mgombea wa tatu wa nafasi hiyo Maryrose Majinge aliambulia kura…
Simba, Bhanj wazozana
Hata hivyo, uchaguzi huo ulinusurika kuingia dosari baada ya mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhanj, kuchafua hali ya hewa ambapo yeye na mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Simba nusura wapigane.
Hata hivyo, uchaguzi huo ulinusurika kuingia dosari baada ya mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhanj, kuchafua hali ya hewa ambapo yeye na mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Simba nusura wapigane.
Katika tukio hilo, Shyrose na Simba huenda wangepigana kutokana na kila mmoja kutaka kuonyesha ubabe kwa mwenzake.
Hali
hiyo ilitokea baada ya Bhanj kuelekeza tuhuma za moja kwa moja kwa
Simba kuwa katika kipindi chake cha uongozi, hakusimama katika majukwaa
kuisaidia CCM hata siku moja.
Kauli hiyo ilionekana kumkwaza
Simba, aliyekuwa jukwaani akijieleza na baada ya kushuka alikwenda moja
kwa moja mahali alipokuwa ameketi Bhanj na kumnyooshea kidole akisema:
“Huniwezi wewe!”
Kauli hiyo ilimkasirisha Bhanj na kufanya ahamaki. Aligeuka na kuuliza: “What! Uko na mimi?”
Ilikuwa
kama sinema, kwani awali, Bhanj alitoka katika kiti alichoketi na
kwenda kukaa mbele, alipokuwa ameketi Sophia Simba, ili aweze kupata
nafasi ya kuuliza maswali.
Awali Bhanj alimuuliza mgombea Anne Kilango Malecela akitaka kujua kilichomsukuma kugombea uenyekiti wa UWT.
Hata
hivyo, swali hilo lilikataliwa na aliyeongoza mkutano huo akiwa
msimamizi wa uchaguzi huo, Profesa Anna Tibaijuka akisema halikuwa na
mashiko.
Hata hivyo, Bhanj aliomba nafasi tena, kabla ya kuipata
ya kumuuliza Simba, Tibaijuka aliwaelekeza kuwa, aulize swali na siyo
kutoa hotuba.
“Mheshimiwa mjumbe, naomba uulize swali siyo kutoa
hotuba, tafadhali naomba apewe nafasi ya kuuliza swali maana naamini
pia mgombea wetu ni mahiri atalijibu tu,” alisema Tibaijuka, kauli
iliyotafsiriwa na baadhi ya wajumbe kuwa ni ya kumbeba Simba.
Akijibu
swali hilo Simba alisema: “Huyu mjumbe, hajui kabisa kampeni za chini,
hizo kelele za wajumbe zinaonyesha kuwa nilikuwa nafanya kazi
kikamilifu, ndiyo maana hata yeye amekuwa ni Mbunge wa Afrika Mashariki
kupitia sisi wanawake.”
Majibu ya Simba yalilipua kelele kutoka
kwa wajumbe ambao moja kwa moja walianza kumshangilia licha kuwa awali
ilikatazwa kufanya hivyo.
Baada ya kumaliza kujieleza na kuomba
kura, ndipo Simba alishuka kuelekea mahali alipoketi na Bhanj alisimama
akitaka kumpisha, lakini ghafla Simba akamnyooshea kidole na kumweleza
kuwa hatamuweza.
Ndipo wakaanza kujibizana na kusababisha mkutano
huo kusimama kwa muda, huku wapambe waliodaiwa kuwa wa Sophia Simba
wakionekana kukerwa zaidi na kutaka kumpiga Bhanj, aliyesaidiwa na watu
wa usalama kuondolewa eneo hilo.
Hata hivyo, Profesa Tibaijuka alizuia watu wa usalama wasimtoe nje Bhanj kwa sababu ni mjumbe halali wa mkutano huo.
Simba ajieleza
Akijieleza katika mkutano huo wa uchaguzi, Simba aliwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT kutochagua watu aliodai kuwa, wakiwa bungeni wanabwatuka ovyo na kuikosoa CCM kana kwamba yuko upande wa upinzani.
Simba ajieleza
Akijieleza katika mkutano huo wa uchaguzi, Simba aliwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT kutochagua watu aliodai kuwa, wakiwa bungeni wanabwatuka ovyo na kuikosoa CCM kana kwamba yuko upande wa upinzani.
“Wajumbe
wa kata, wilaya na mikoa mmekuwa mkifuatilia habari za Bunge kila
wakati, nadhani mnaona, mimi ni Serikali siwezi kubwatuka ovyo. Lakini
kuna watu wanabwatuka na kusema patachimbika, huku wakikikosoa chama.
Hawafai hao,” alisisitiza Simba.
Miongoni mwa wagombea watatu wa
nafasi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, wawili ni wabunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ambao ni Simba na Kilango Malecela na ambao
wamekuwa wakisigana katika kampeni, huku Maryrose Majinge akionekana
kutotajwa.
Kauli ya Simba ilionekana wazi kumwelekea Kilango,
ambaye mara zote amekuwa akijipambanua kuwa mpambanaji wa ufisadi na
kuonekana kama mtetezi wa wanyonge.
Tofauti na maelekezo ya
mwenyekiti wa muda na msimamizi wa uchaguzi huo, kauli hiyo ya Simba
iliibua kelele za kuzomea na kushangilia wakiimba Simba, Simba, Simba.
Simba
alikanusha kuwa, suala la ukomo wa Viti Maalumu halijafika kwa nafasi
za udiwani bali lipo kwa wabunge na kwamba litajadiliwa kwenye maoni ya
Katiba Mpya.
Nje ya ukumbi wa mikutano, Simba alisimama mlangoni akiomba kura kwa kila mjumbe aliyekuwa akiingia ukumbini.
Kilango ajinadi na Biblia mkononi
Tofauti na hasimu wake, mgombea Anna Kilango Malecela alifika katika ukumbi wa mikutano akiwa katika gari moja na mumewe Malecela na kuingia moja kwa moja ukumbini.
Tofauti na hasimu wake, mgombea Anna Kilango Malecela alifika katika ukumbi wa mikutano akiwa katika gari moja na mumewe Malecela na kuingia moja kwa moja ukumbini.
Mara baada ya kushuka katika gari, wanandoa hao
walikumbatiana na kisha Malecela alionyesha ishara ya mkono ili mkewe
aingie ndani ya ukumbi naye alitekeleza.
Akiwa ndani ya ukumbi, Kilango alipita kila kiti na kuwaomba wajumbe kura huku akiwa amebeba Biblia mkononi.
Haikujulikana
ni kwa nini Kilango alitumia staili hiyo ya kuwa na Biblia, lakini
baadhi ya wajumbe walitafsiri kuwa ilikuwa ni kuonyesha kuwa anamtegemea
Mungu kwa kila kitu.
Katika hotuba yake ya kuomba kura, alisema
kuwa, atahakikisha kuwa UWT inawezeshwa kiuchumi pamoja na kuwasaidia
watendaji wa ngazi za wilaya kuishi na wenza wao.
Kilango
aliwaeleza wajumbe namna alivyo na mvuto na ubavu wa kupambana na
upinzani, hasa katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015, akipewa nafasi
hiyo anaweza kusambaratisha ngome zote za upinzani.
Alitoa mfano
wa kiwanda cha kusindika tangawizi alichojenga katika Jimbo lake la Same
Mashariki kuwa, alipopewa nafasi ya ubunge alihakikisha kuwa
anafanikisha mambo mengi.
Kilango aliahidi kuongeza kipato cha watendaji wa nafasi mbalimbali ndani ya UWT, ili waweze kuwa na kipato cha kuwatosha.
Maryrose Majinge
Kwa upande wake, Majinge alifika katika mkutano na kuingia moja kwa moja ndani ya ukumbi na kuanza kuomba kura kwa wajumbe mmoja, mmoja waliokuwa wakiingia ndani ya ukumbi.
Kwa upande wake, Majinge alifika katika mkutano na kuingia moja kwa moja ndani ya ukumbi na kuanza kuomba kura kwa wajumbe mmoja, mmoja waliokuwa wakiingia ndani ya ukumbi.
Katika hotuba yake mgombea huyo aliwataka wajumbe kuchagua viongozi wenye ushawishi na si watu wa mavazi.
“Nina uwezo wa kushawishi, nina elimu ya kutosha kuongoza na ninatosha kimaadili pia. Ninaomba mnichague, maana uongozi siyo mavazi ya kanga na vitenge wala nyimbo,’’alisema Majinge.
“Nina uwezo wa kushawishi, nina elimu ya kutosha kuongoza na ninatosha kimaadili pia. Ninaomba mnichague, maana uongozi siyo mavazi ya kanga na vitenge wala nyimbo,’’alisema Majinge.
Nje ya ukumbi
Njeya ukumbi wa mkutano huo mkuu wa UWT, kambi mbili zilikuwa zikitambiana kwa nyimbo za mafumbo na ushangiliaji.
Njeya ukumbi wa mkutano huo mkuu wa UWT, kambi mbili zilikuwa zikitambiana kwa nyimbo za mafumbo na ushangiliaji.
Wapambe
wengi waliokuwa wanaume waliokuwa wamevalia mabango ya picha ya Simba
huku wakiimba; “Simba lazima aungurume leo Dodoma.”
Kwa upande wa wapambe wa Kilango walikuwa wakiimba; “Tunataka mabadiliko, tunataka mabadiliko.”
Hata hivyo kundi la Kilango lilionekana kuwa ni dogo.
Hata hivyo kundi la Kilango lilionekana kuwa ni dogo.
Rushwa nje nje
Uchaguzi huo uligubikwa na viashiria vyote vya rushwa ingawa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilionekana kuweka mitego yake kila kona.
Uchaguzi huo uligubikwa na viashiria vyote vya rushwa ingawa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilionekana kuweka mitego yake kila kona.
Hata hivyo, kulikuwa na mbinu za hali ya juu ambapo baadhi
ya wajumbe walikuwa wakichukulia pesa kwa wauza nguo pamoja na vibanda
vya mama lishe, ambao jana ilikuwa siku ya mavuno kwao.
“Mimi
nimeelekezwa majina ya watu, kwa hiyo wakifika katika eneo hili
wanajitambulisha na ninawapa elfu ishirini. Lakini lazima na mimi
nihakikishe kuwa nabakiwa na pesa, maana wengine nawapa hata elfu kumi
na wengine naona hawaji kabisa,” alisema mmoja wa wauza vyakula nje ya
ukumbi huo.
Mama huyo alisema kuwa hakujua pesa alizokuwa akitoa
zilikuwa ni za upande wa mgombea gani, lakini alikubali kuzishika kwa
kuwa watu hao walinunua pia chakula chake chote.
Mamalishe huyo
alisema baadhi ya wapambe waliokuwa wamesimama mahali pa wazi kuonyesha
ishara ya wajumbe wanaostahili kupewa posho hizo.
Alibainisha hayo
baada ya mwandishi wa habari hizi kumaliza kula chakula na alipotakiwa
kulipa ndipo mama huyo alipobaini kuwa hakuwa miongoni mwa wapambe na
akakataa kuzungumza zaidi.
Awali akifungua Mkutano huo Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilali,
aliwataka wajumbe kuchagua viongozi waadilifu.
Dk Bilali alisema
iwe mwiko kuwachagua watu waliotoa rushwa kwa ajili ya kununua uongozi
ma kutahadharisha kuwa jambo hilo linaweza kuwa ni shubiri kwa CCM.Via mwananchi
No comments:
Post a Comment