SERIKALI imepiga marufuku mihadhara ya kidini nchi nzima kwa siku 30
ikiwa ni moja ya hatua ya kukabiliana na machafuko ya kidini
yanayolinyemelea taifa.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel
Nchimbi alitangaza hatua hiyo ya Serikali jijini Dar es Salaam jana,
wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Waziri Nchimbi
alisisitiza kuwa Serikali pia inafanya uchunguzi ili kubaini kama
vurugu hizo zina mkono wa makundi ya nje ya nchi.
Alisema kuwa,
Serikali sasa haitawabembeleza watu wanaoeneza chuki za kidini kwa
sababu ni wajibu wake kulinda amani kwa wananchi wake.
Waziri
huyo alieleza kusikitishwa na vurugu zilizotokea juzi Ijumaa maeneo
mbalimbali jijini baada ya baadhi ya Waislamu kujiandaa kuandamana
kwenda Ikulu kushinikiza kutolewa rumande kwa kiongozi wao, Sheikh Issa
Ponda.
Waandamanaji hao pia walipinga tukio la kukojolewa kwa
kitabu kitakatifu cha Kurani na mtoto lililotokea mwanzoni mwa wiki eneo
la Mbagala.
“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametangaza juzi
kusitisha mihadhara ya nje kwa siku 30. Na mimi natumia fursa hii
kutangaza kusitisha mihadhara hiyo kwa nchi nzima kwa siku 30, hadi
tutakapoona hali imetulia,” alisema Nchimbi.
Waziri Nchimbi
alikiri pia kwamba, Serikali imekuwa ikikosea kuwakamata watu wanaofanya
vurugu wakati wa maandamano na kuwaacha wanaoshawishi na kuwezesha
maandamano hayo.
“Huo ndiyo uamuzi mpya wa Serikali.
Anayeshawishi, anayefanikisha na anayewezesha, wote watakamatwa.
Tumegundua kwamba, tulikuwa hatufuati sheria kwa kuwakamata tu
wanaotenda. Ndiyo maana baada ya upelelezi tukaona kuwa wasaidizi wake
(Ponda), waliwashawishi watu waandamane kwenda Ikulu ,au gerezani ili
wamtoe (Ponda) rumande,” alisema Dk Nchimbi.
Alipongeza Mwananchi
Katika hatua nyingine, Waziri Nchimbi alilimwagia sifa gazeti la Mwananchi kwa tahariri zake zinazohimiza kudumishwa kwa amani, hasa baada ya matukio ya uvunjifu wa amani, ikiwamo kuchomwa moto na kuibwa kwa mali za makanisa hivi karibuni.
Katika hatua nyingine, Waziri Nchimbi alilimwagia sifa gazeti la Mwananchi kwa tahariri zake zinazohimiza kudumishwa kwa amani, hasa baada ya matukio ya uvunjifu wa amani, ikiwamo kuchomwa moto na kuibwa kwa mali za makanisa hivi karibuni.
Katika tahariri yake ya jana
iliyochapishwa ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa cha habari ‘Chonde
chonde tunaomba amani’, gazeti hili lilionya juu ya uwezekano wa
kuvunjika kwa amani na likataka pande zinazohusika kujiepusha na matukio
yanayoweza kulitumbukiza taifa katika machafuko.
Waziri Nchimbi
alisisitiza kuwa Serikali inafuata utawala wa sheria, hivyo haitaruhusu
watu kufanya maandamano kwenda popote ili kushinikiza kumtoa mahakamani
mtu aliyetuhumiwa hadi mahakama itakapotoa uamuzi wake.
“Mahakama peke yake ndiyo yenye mamlaka ya kutoa hati ya mtu, hivyo kujaribu kumtoa mtu aliyefikishwa mahakamani ni kosa kisheria,” alisisitiza.
“Mahakama peke yake ndiyo yenye mamlaka ya kutoa hati ya mtu, hivyo kujaribu kumtoa mtu aliyefikishwa mahakamani ni kosa kisheria,” alisisitiza.
Huku
akitaja mifano wa baadhi ya nchi duniani ambazo zimewahi kukumbwa na
machafuko ya kidini, Dk Nchimbi alisema kuwa Serikali haitavumilia mtu
au kikundi chochote kitakachoonekana kikieneza chuki za kidini.
“Staili
yetu ya kucheka na wavunja amani inatuharibia. Kwetu sisi amani ni
muhimu mno….Wote mnajua jinsi chokochoko za kidini zilivyoleta madhara
nchini Nigeria, hakuna anayetaka kwenda tena huko, watu zaidi ya
milioni mbili waliuawa. Migogoro ya dini iliwahi kuzikumba nchi za Ulaya
miaka 400 iliyopita na kusabanisha vifo vya watu milioni nne,” alisema
na kuongeza:
“Huko Lebanon, Waislamu wa madhehebu ya Sunni
walikuwa wakigombana na Wakristo. Hadi wanakuja kutafuta suluhisho
tayari watu 250,000 walikuwa wameuawa… Hivi kweli Watanzania na sisi
tutasubiri hadi watu milioni tisa wafariki, mali ziharibiwe halafu ndiyo
tujadiliane?”
Dk Nchimbi amewaonya wanasiasa kutochukulia vurugu
hizo kwa masilahi ya kisiasa, huku akiwataka wananchi na vyombo vya
habari kutoshabikia uvunjifu wa amani.
Kuhusu vyombo vya habari
vya kidini vinavyoeneza chuki alisema Serikali itaiwajibisha Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA) na taasisi nyingine za Serikali zinazosimamia, endapo
kutakuwa na redio au televisheni na magazeti yanayoeneza maneno ya
chuki za kidini.
Akizungumzia suala la kuonekana kwa kiongozi wa
kundi la Uamsho la Zanzibar Sheikh Farid Hadd, Dk Nchimbi alisema kuwa
baada ya kuonekana huko jeshi la polisi limemkamata na linamhoji ili
kujua alikokuwa na kwa nini alipotea na kusababisha wafuasi wake wafanye
vurugu iliyosababisha pia kuuawa kwa askari polisi wa kikosi cha
kutuliza ghasia.Chanzo cha habari na Mwananchi
No comments:
Post a Comment