EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, October 28, 2012

TAKUKURU ndiyo vinara wa rushwa.

Habari hii imeandikwa na Happiness Mnale via Tanzania Daima

WABUNGE wameigeuzia kibao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa ndiyo inaongoza kwa vitendo vya rushwa.

Wakizungumza kwa jazba jana jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa, ikiwa ni harakati ya mapambano ya rushwa, wabunge hao waliwashutumu vikali watendaji wa TAKUKURU na kuwatupia lawama kuwa ni vinara wa rushwa.Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Assumpter Nshiyu Mshama, alisema kuwa TAKUKURU ndio wala rushwa wakubwa, huku akiwataka wabunge kuamua rushwa iishe kwani inawezekana.

Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, alisema kuwa rushwa iko kila mahali, lakini kikubwa TAKUKURU watakasike, kwani wao ndio wanaoongoza kwa kukumbatia rushwa, “TAKUKURU wao ndio vinara wa rushwa. Kwa mfano katika uchaguzi uliopita wakati wa kampeni ukiwapigia simu kuna rushwa sehemu fulani wao ndio wanakuwa wa kwanza kuwapigia watoa rushwa wakimbie eneo husika, baadaye wanajifanya kwenda na kukwambia hakuna wala rushwa, wajitakase wao kwanza,” alisema Msigwa.Hata hivyo Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy, alizitupia lawama nchi za Magharibi kwa kukumbatia wala rushwa, hasa wanaoficha fedha benki za nje, “Mataifa yaliyoendelea ndio waficha rushwa, ni wabaya sana, watu wanaweka fedha katika mabenki ya Ulaya nao wana wakumbatia, kesi za TAKUKURU hakuna hata moja serikali imeshinda, ifike wakati mwenye mali kuliko uwezo wake akamatwe,” alisema Keissy.

Pia Keissy alisema kuwa TAKUKURU wanatakiwa watende haki katika suala zima la rushwa, ikiwemo kuacha kuwakumbatia na kuwasafisha wala rushwa.Katika hatua nyingine, wabunge hao waliijia juu TAKUKURU kwa kutoa chapisho linalomuonesha Mbunge wa Bahi, Omari Badwel, ambaye anatuhumiwa kwa rushwa wakidai kuwa ni kuingilia Mahakama.

Akijibu shutuma hizo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mashitaka TAKUKURU, Donasian Kessy, alisema watalifanyia kazi suala hilo, ikiwamo kuwataka wabunge wasiiogope TAKUKURU pindi wanapokuwa na ushahidi.Kessy pia alisema kuwa tayari TAKUKURU wameshawakabidhi Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba mapendekezo mapya ya sheria kuhusiana na rushwa.Akizungumzia utoaji wa picha ya Badwel, Kessy alisema kuwa picha hiyo haijengi mazingira ya kuingilia uhuru wa Mahakama na utendaji kazi wake, bali ni moja ya matukio yaliyotokea katika kipindi cha mwezi Aprili, mwaka huu, hivyo ni kawaida kwa TAKUKURU kuchapisha matukio hayo.

Awali akiwasilisha mada katika semina hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Andrew Mbwambo, alisema kuwa vyama vya siasa vinatakiwa kujiendesha kwa haki, si rushwa, ikiwamo kuacha uchakachuaji.Pia alisema kuwa uchaguzi wa ndani wa vyama unatakiwa utungiwe sheria ya kuzuia rushwa, ikiwamo kutochaguana kwa kuheshimiana, bali waangalie uwezo wa mtu.Prof. Mbwambo pia aliwataka wabunge hao kutambua umuhimu wa wanahabari, hivyo hawapaswi kuwafukuza wala kuwaogopa pindi wanapotimiza wajibu wao.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate