EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 24, 2012

WANAWAKE VIJANA 10 WALIOONESHA NJIA.


UPO msemo uliotawala vichwa vya watu tangu dahari kwamba wanawake ni tabaka la kukaa nyumbani na kufanya kazi za ndani. Wao jukumu lao ni kumfurahisha mume na lingine ni kuwaandaa watoto kwa ajili ya kwenda shule na kufuatilia nyenendo zao darasani.
 
Happiness Magesse.
Ilivyozoeleka ni kwamba wanawake ni goigoi. Utaona bungeni kuna wabunge wa viti maalum ambavyo wengi hutafsiri kuwa ni vya upendeleo. Kwa maana kwamba uwezo wao kushindana kwenye majimbo na kushinda ni mdogo ndiyo maana wanapewa hivyo maalum kwao.
Katika mitihani, kuna unafuu wa alama za ufaulu kwa wanafunzi wa kike. Yaani wanaonekana hawana uwezo wa kushindana na wavulana. Vijijini, wanawake wamekuwa wakitumika kama nyenzo ya kilimo, yaani mama akalime ndiyo alishe familia, baba akacheze bao au kunywa pombe.
Miaka inakwenda, wapo wanawake wengi ambao wameweza kudhihirisha kwamba inawezekana kwa jinsi ya kike kuanzisha kazi na kufanikiwa. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ni mfano wenye nguvu kwa wanawake kufanikiwa.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mchungaji Getrude Rwakatare na wengineo, ni kichocheo kinachotoa uthibitisho kuwa wanawake wanaweza. Ni suala la kuwaamini na kuwapa nafasi, kwa hakika wanaweza kufanya mambo makubwa mno.
Ukiachana na hao, ipo orodha ya wanawake vijana 10 ambao wanastahili pongezi. Wamepambana katika maeneo yao kiasi cha kupata mafanikio ambayo yameonesha njia. Inabidi tuwatambue na kuthamini jitihada zao kwa maana wameendelea kuthibitisha ndivyo sivyo kwa wale waliokuwa wanaamini kuwa wanawake si lolote kwenye utafutaji.
SUSAN MASHIBE
Ni mwanamke jasiri, mpiganaji mwenye utaalam wa masuala ya anga aliyethibitishwa na Mamlaka ya Anga Marekani (FAA). Anamiliki Kampuni ya TanJet inayojihusisha na utoaji wa ushauri wa masuala ya anga ndani na nje ya nchi.
Mwaka jana, alinukiwa Tuzo ya Kiongozi Kijana Ulimwenguni (Global Young Leader), aliyopewa na Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF). Kampuni yake imekuwa ikipata tenda mbalimbali barani Afrika, Ulaya, Marekani na kadhalika. Jopo la wajumbe wa Baraza la Congress nchini Marekani, lilipotembelea Tanzania mwaka 2009, Mashibe ndiye aliyeratibu masuala ya anga kuhusu ujio wao.
FLAVIANA MATATA
Mwaka 2007 alipokwenda kushiriki mashindano ya dunia ya Miss Universe na kushika nafasi ya sita, wengi walidhani huo ndiyo mwisho wake. Ilionekana hivyo kwa sababu warembo wengi wameshiriki mashindano ya dunia na baada ya kurudi nchini, hawakusikika tena.
Kwa Flaviana, huo ulikuwa ni mwanzo wa kupiga hatua zaidi kusaka mafanikio yake. Hivi sasa, mrembo huyo ni mwanamitindo wa kimataifa, anayefanya kazi na makampuni makubwa ulimwenguni.
 
HAPPINESS MAGESSE
Miss Tanzania aliyechukua taji hilo mwaka 2001, Happiness Magesse ndiye aliyefanikiwa zaidi kimataifa kuliko wote, japo wapo wengine wanaojitahidi. Hivi sasa Happiness ‘Millen’ ni mwanamitindo wa kimataifa.
 
EMELDA MWAMANGA
Ni mwanzilishi aliye pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Relim Entertainment inayomiliki jarida maarufu la Kiingereza, Bang. Jinsi alivyoweza kulisimamisha jarida hilo na kulifanya kuwa maarufu zaidi nchini, inatosha kumpongeza kwamba ameonesha njia.
 
LADY JAYDEE
Jina lake asilia ni Judith Wambura. Ni mwanamuziki wa kike mwenye mafanikio zaidi ambayo chanzo chake ni muziki. Anamiliki bendi na mgahawa wa kisasa ambao ulimgharimu zaidi ya shilingi milioni 100 kuuanzisha. Bila shaka Jaydee ameonesha njia kwa wanamuziki wengine wa kike hapa nchini.
 
MADAM RITA
Kuanzisha kitu wakati mwingine inaweza kuwa jambo rahisi lakini uimara wa mtu ni pale anapoweza kulisimamia na kufanikiwa. Rita Paulsen anastahili pongezi kwa namna alivyoweza kuanzisha Shindano la Bongo Star Search na kulifikisha hapa lilipo. Huyu ni mwanamke kijana aliyeonesha njia ya kweli ya mafanikio.
 
RAHMA AL-KHAROOS
Anamiliki Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology. Uwezo wake uliweza kuwashtua wengi pale alipoweza kujitolea mamilioni ya fedha kuiwezesha Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars. Mwanamke huyu ni mfano tosha kwamba inawezekana kama tu utaamua kupambana.
 
SHEAR NASSA
Anamiliki maduka ya Shear Illusions, vilevile ana jarida linaloitwa Shear Hair & Beauty. Ukubwa wa maduka yake, heshima na umaarufu wake kwa uuzaji wa vitu vya urembo ni kielelezo cha kumthibitisha Shear kwamba ni mwanamke kijana aliyefanikiwa, kwa hiyo ameonesha njia.
 
KHADIJA MWANAMBOKA
Mbunifu wa mavazi wa kike mwenye umaarufu kuliko wanawake wote nchini. Ameanza harakati zake akiwa na umri mdogo na kwa alipofikia hivi sasa, ameshaonesha njia kwa wanawake wengine nchini. Jambo muhimu ni kusimamia fani yako mpaka kuifikisha kwenye kiwango bora. Khadija alipofikia kwa ubunifu wa mavazi, anastahili pongezi.
 
FINA MANGO
Alipata umaarufu mkubwa kwenye fani ya utangazaji wa redio lakini alipoamua kuanzisha kampuni yake ya One Plus, ameweza kupata mafanikio makubwa. Tenda ya kuratibu na kusimamia Tuzo za Muziki Tanzania (Tuzo za Kili) kwa miaka mitatu mfululizo imedhihirisha ubora wa kampuni yake.
Kumradhi, makala ya pasua jipu, itaendelea wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate