SWEDEN wakiwa nyumbani jana usiku waliitandika Uingereza 4-2 katika mchezo mkali wa soka wa kirafiki.
Mtu aliyepeleka kilio kwa Waingereza ni mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic aliyefunga mabao yote manne.
Hiki
kinakuwa ni kipigo cha kwanza tangu Roy Hodgson achukue nafasi ya
kuikochi Uingereza na ni mara ya kwanza pia kwa taifa hilo kufungwa
mabao manne na mtu mmoja.

Ibrahimovic
alianza kufunga goli mwanzoni kabisa mwa mchezo kabla ya Uingereza
haijapata mabao mawili kupitia kwa Welbeck na Steven Caulker na kufanya
Sweden iwe nyuma kwa 1-2 hadi mapumziko.
Mabao
matatu yaliyofungwa na Ibrahimovic katika ngwe ya pili yalikuwa ni
shubiri tosha kwa nahodha wa Uingereza Stephen Gerald aliyekuwa
akifurahia kutimiza mechi ya 100 kwa taifa lake.Via www.saluti5.com
No comments:
Post a Comment