EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, November 14, 2012

HII NDO HISTORIA YA MAREHEMU MARIAM KHAMIS, SOMA KILA KINACHOMUHUSU HAPA.

           CHANZO CHA HABARI NA SALUTI5- www.saluti5.com
WENGI wamezipokea kwa mshituko taarifa za kifo cha mwanamipasho Maariam Khamis “Paka Mapepe" (26), aliyefariki wakati wa kujifungua kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana alfajiri.
Hiyo ni kwasababu, Paka Mapepe alikuwa kivutio kikubwa na kipenzi cha wengi, hasa kutokana na uimbaji wake uliojaa hisia nzito, kwenye tungo zote alizoimba.Hadi mauti yanamfika, Paka Mapepe alikuwa yu msanii wa kundi la mipasho la TOT Taarab lililop0 chini ya chama tawala CCM.
Alijiunga na TOT Taarab mwanzoni mwa mwaka jana, akitokea katika kundi la Five Stars Modern Taarab aliloingia mwishoni mwa mwaka 2009.
Paka Mapepe aliipa kisogo Five Stars na kuhamishia virago TOT  Taarab muda mfupi kabla ya ajali ya kundi hilo iliyoua wasanii 13, Machi, mwaka jana, Mikumi Morogoro.
Akiwa Five Stars, alitikisa vilivyo kwa vibao viwili; ‘Ndo Basi Tena’ pamoja na ‘Uzushi Wenu Haunitii Doa’ .
www.saluti5.com iliwahi kuongea naye wakati wa uhai wake, kuhusiana na msiba wa wasanii wenzake wa Five Stars, ambako alisema kuwa, ni msiba uliogonga kwa kishindo moyoni mwake.

Mara kwa mara alikuwa akiweweseka na kuwaota baadhi ya marehemu wasanii wa Five Stars, kila alipokumbuka namna alivyoishi nao vema,hata pale alipobadili upepo na kuingia TOT  Taarab.
Historia yake kimuziki ilianzia mwaka 2003, mara baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, ambako alipenda sana Taarab, kwa kuvutiwa na magwiji wa mipasho.
Baadhi ya magwiji hao waliokuwa wakimvutia Paka Mapepe ni pamoja na Zuhura Shaaban, ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa na marehemu Nasma Khamis ‘Kidogo’.
Wakati huo, kutokana na shetani muziki kumpanda kindakindaki kichwani kwake, alikuwa akiandika kwenye daftari mashairi ya baadhi ya vibao vyao na kuviimba mara kwa mara kila alipotulia.
Kati ya watu waliogundua mapema kipaji chake cha uimbaji na kukifanyia kazi, ni baba yake mdogo aitwaye Kessy Abdallah ambaye alimuunganisha kwenye kundi la Segere No2, jijini Dar es Salaam, ili kujifua zaidi.
Akiwa Segere, ambalo baadhi ya vinara wake alikuwa Mussa Msuba,
alirekodi kibao kiimoja kinachokwenda kwa jina la ‘Mpenzi Wana kabla albamu yake haijatoka, kundi lilisambaratika.
Mwaka 2007, Mussa Mipango, kati ya wacharazaji mahiri wa gitaa zito, Besi hapa nchini, aliyeko TOT Taarab hivi sasa, alimuunganishia katika kundi la Zanzibar Stars Modern Taarab ‘Watoto wa Pwani’.
Hakukaa sana Zanzibar Stars kwani mwaka huohuo, 2007 alitimkia East African Melody Taarab alikorekodi kibao ‘Paka Mapepe’ kilichotokea kutikisa vilivyo kiasi cha mashabiki kuamua jina hilo liwe la kwake moja kwa moja.
Mwaka 2008, Paka Mapepe alirejea Zanzibar Stars alikofikia kurekodi kibao ‘Huliwezi Bifu’, kabla ya vingine kama vile; ‘Raha ya Mapenzi’, ‘Narindima Mie’ na ‘Shoga Habari Ndo Hiyo’ .
Kila wakati, Paka Mapepe alikuwa akikiri kuwa, ujuzi wake kiuimbaji ulikuwa unatokana na kutilia mkazo madrasa ya Shadria, jijini Dar es Salaam, alikosoma na kufikisha juzuu mbili.
Mara tu baada ya kuingia TOT  Taarab, Paka Mapepe alipewa kurekodi kibao ‘Sidhuriki na Lawama’, ambacho hata mwenyewe alikuwa akithibitisha kuwa, kilitokea kumsogeza na mashabiki wengi wa mipasho.
Kati ya watu ambao mara kwa mara alipenda kuwataja kuwa ni miongoni mwa waliochangia kumfikisha alipoishia, ni pamoja na baba na mama yake waliompa moyo tangu alipoanza kujiingiza katika muziki.
Aidha, alikuwa pia akipenda kuvishukuru vikundi vyote vya muziki wa taarab alivyopitia ikiwamo Melody na mashabiki pamoja na wapenzi wote kwa ujumla.
Aliolewa na mcharazaji mahiri wa gitaa la Besi, Haji Kijungu, aliyejaliwa kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Taliq (6).
Paka Mapepe alizaliwa mwaka 1986, jijini Dar es Salaam na kupata elimu ya msingi katika shule ya Amana, Ilala kuanzia mwaka 1994 hadi 2000 na sekondari ya Jamhuri kati ya mwaka 2001 na 2003.

MAZISHI ya mwimbaji Mariam Khamis aliyefariki jana alfajiri yatafanyika leo, Magomeni jijini Dar es Salaam.
           MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate