MWIGIZAJI
Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’
amewashutumu wasanii wenzake kwa kusema uongo katika jamii kuhusu maisha
yao halisi sambamba na malipo wanayopata katika filamu wanazoshiriki.

Msanii
huyo amedai kwa kufanya hivyo wasanii wengi wemejikuta katika maisha ya
kuunga unga kutokana uongo huo. “Baadhi ya wasanii wa filamu
wanadanganya sana kuhusu hali halisi ya maisha yao, mtu akipata nafasi
ya kuongea na vyombo vya habari kuhusu malipo na maisha yake halisi
utakuta akisema kuwa yeye bila kulipwa milioni tano hawezi kushiriki
katika filamu, lakini ukweli hakuna msanii wa kawaida anayelipwa fedha
kama hizo katika tasnia ya filamu Bongo mimi mwenyewe ni mtayarishaji
”anasema Monalisa.
Anaendelea
kudai kuwa kufuatia udanganyifu huo Serikali kupitia Bodi ya filamu
iliamua kuongeza gharama za kibali cha kurekodi filamu hadi kufikia laki
tano jambo lilofanya wasanii walalamike kuwa ni fedha kubwa sana
kulingana na malipo ya filamu, lakini ilitokana na udanganyifu kutoka
kwa baadhi ya wasanii wa filamu kudanganya, mwanadada huyo anasema hali
ya soko la filamu ni mbaya kwa sasa.
Habari imetoka www.filamucentral.co.tz
No comments:
Post a Comment