EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, November 11, 2012

NANI ZAIDI CHELSEA V LIVERPOOL? SOMA DONDOO MUHIMU HAPA.

LONDON, ENGLAND
CHELSEA itaikaribisha Liverpool katika Uwanja wa Stamford Bridge Jumapili ya leo katika moja ya mechi kubwa za Ligi Kuu England.
Timu hizi zinakutana huku kukiwa na kumbukumbu kuwa Liverpool imeshinda mechi tatu (mbili za Ligi Kuu, moja ya Carling Cup) kati ya nne walizokutana msimu uliopita – mechi pekee waliyoshindwa ni ya fainali ya Kombe la FA.
Liverpool inaonekana kuvutia mchezoni chini ya bosi wao mpya, Brendan Rodgers, lakini bado inashindwa kugeuza mafanikio hayo kuibuka na ushindi katika mechi za Ligi Kuu.
Baada ya mechi 10, imebaki katika nusu ya chini kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imeshinda mara mbili tu na kuwa na pointi 11, huku tatizo lao kuu likibaki kuwa upachikaji mabao.
Liverpool imefanikiwa kutikisa nyavu za adui mara 13 pekee, huku saba kati ya hayo yakifungwa na kinara wao wa ushambuliaji, Luis Suarez.
HABARI ZA CHELSEA:
Roberto Di Matteo bado hatarajiwi kuwa na majeruhi Frank Lampard na kuna shaka pia kama Ashley Cole ataweza kuwa fiti kutoka na maumivu ya misuli ya paja aliyopata katika mechi iliyopita nyumbani kwa Swansea, ingawa hali inaweza kumpa nafasi Ryan Bertrand ya kuanza beki ya kushoto.
Hata hivyo, Roberto ana bahati ya kuweza kumtumia tena John Terry baada ya nahodha huyo wa klabu kumaliza adhabu yake ya kukosa mechi nne aliyopewa kutokana na kutenda vitendo vya kibaguzi kwa Anton Ferdinand.
Mbele, kuna matumaini kwa Fernando Torres kuweza kupiga bao lake la kwanza kwa Chelsea dhidi ya Liverpool baada ya kucheza mechi nne mfululizo bila kutikisa nyavu.
Kikosi cha kwanza kwa Chelsea kinatarajiwa kuundwa na Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Bertrand, Mikel, Ramires, Oscar, Hazard, Mata na Torres.
Mchezaji wa kuchunga: Oscar ni mmoja wa wachezaji waliotokea kupiga mabao makali Chelsea, lakini bado ukweli unabaki kuwa yeye si kila kitu. Kinda huyu amekuwa akijitoa kusaidia timu, sasa je, ataweza kupiga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu?
HABARI ZA LIVERPOOL
Brendan Rodgers anarudi kwa mara ya kwanza Stamford Bridge, kama kocha wa Liverpool. Hakuna shaka kwamba atakuwa akitafuta kufanya kweli mbele ya mwajiri wake wa zamani (aliwahi kuwa kwenye benchi la ufundi la Chelsea enzi za Jose Mourinho), lakini anakabiliwa na jaribio zito.
Baada ya kupumzisha mastaa kadhaa wenye majina kwenye mechi ya Europa League usiku wa Alhamisi iliyopita, Rodgers anatarajiwa kutumia kikosi madhubuti kwa ajili ya mechi hii.
Anayetarajiwa kurejea kutoka kuwa majeruhi ni beki wa zamani wa Chelsea, Glen Johnson. Hata hivyo mchezaji mwingine wa zamani wa Chelsea, Fabio Borini, yupo kwenye orodha ya majeruhi.
Mchezaji wa kuchunga: Luiz Suarez ni mchezaji mmoja wa Liverpool mwenye uwezo wa kuuweka mchezo kwenye himaya yake. Si kila siku inakuwa njema kwake, lakini akiamka vizuri, anakuwa injinia wa kweli wa ushindi.
DONDOO ZA MECHI NA TAKWIMU:
Kisasi ni kitu kilicho kwenye orodha ya mechi ya Jumapili hii. Liverpool ilifanikiwa kufanya kweli mara mbili dhidi ya Chelsea katika Ligi Kuu msimu uliopita.
Katika siku za karibuni, kitabu cha rekodi kinaonyesha kuwa matokeo yako wazi kwa kila timu – hakuna iliyoachwa mbali. Katika misimu nane iliyopita, timu hizi zimekutana mara 32, huku Chelsea ikishinda mara 13 na Liverpool 12.
RATIBA LIGI KUU ZA ULAYA
ENGLAND
Jumapili, Novemba 11, 2012
Man City v Tottenham, saa 11:30 jioni
Newcastle v West Ham, saa 1:00 usiku
Chelsea v Liverpool, saa 2:00 usiku
HISPANIA
Jumapili, Novemba 11, 2012
Valladolid v Valencia, saa 9:00 alasiri
Bilbao v Sevilla, saa 1:00 usiku
Mallorca v Barcelona, saa 2:50 usiku
Atletico v Getafe, saa 4:45 usiku
Levante v Madrid, saa 6:30 usiku
ITALIA
Jumapili, Novemba 11, 2012
Palermo v Sampdoria, saa 9:30 alasiri
Chievo v Udinese, saa 12:00 jioni
Torino v Bologna, saa 12:00 jioni
Genoa v Napoli, saa 12:00 jioni
Parma v Siena, saa 12:00 jioni
Lazio v Roma, saa 12:00 jioni
AC Milan v Fiorentina, saa 12:00 jioni
Atalanta v Inter Milan, saa 5:45 usiku
                               Via www.saluti5.com

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate