MLIMBWENDE Nargis Mohamed amesema hakuna jambo lilimvutia kama lile la yeye kumnyima 'unyumba' Vincent Kigosi maarufu kama Ray.


Akiongea katika kipindi cha Action & Cut kinachorushwa na Channel ten, Nargis alisema katika scene zilizomfurahisha wakati wa utengenezaji wa movie ya Woman of Principle ni zile zilizokuwa zinamuongoza yeye kumnyima tendo la ndoa Ray.
“Unajua kwa sasa mimi ni mke wa mtu, kuna vitu vinakuwa vigumu kuviigiza lakini kwa kweli zile za mimi kumnyima unyumba Ray zilinifurahisha sana, alisema Nargis aliyewahi kuwa Miss Tanzania No. 2 miaka kadhaa iliyopita.
Katika Movie hiyo Nargis aliigiza kama mke mtata wa Ray ambapo mara kadhaa alioneka kumtolea nje mumewe kila alipohitaji tendo la ndoa.
CHANZO CHA HABARI NI SALUTI5 (www.saluti5.com).
No comments:
Post a Comment