VIONGOZI
wapya wa Chama cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA), wanatarajiwa
kutambulishwa leo katika tukio
litakalohusisha mechi kadhaa za netiboli baina ya timu zilizopo mkoani humo.
Kwa
mujibu wa Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa CHANEDA, Michael Maurus, utambulisho
huo utaanza saa nane mchana kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini, jijini Dar es
Salaam.
Alizitaja
timu zitakazopambana katika utambulisho huo kuwa ni Kaza Roho ya Kiwalani na
Majumba Sita ya Ukonga (wanaume), huku pia zikiwamo timu za watoto ambazo ni
Kiwalani Kids na Ukonga Kids.
“Kwa
upande wa timu za wanawake, zilizothibitisha kushiriki ni Uhamiaji, Bandari
Queens A, Bandari Queens B, CBE na Chuo Kikuu cha Tumaini,” alisema Maurus.
Aliwataja
viongozi watakaotambulishwa siku hiyo baada ya uchaguzi uliofanyika mwezi
uliopita kuwa ni
Winfrida
Emmanuel (Mwenyekiti), Pili Mogella (Makamu Mwenyekiti), Joseph Ng’anza (Katibu
Mkuu), Christina Kimamla (Katibu Msaidizi), Anitha Lunogela (Mhazini) na
Maurus.
Maurus
aliwataja wajumbe kuwa ni Khadija Ally, Zainab Seif, Georgina Kasembe na
Mussa
Sambala ambapo aliwataka wadau wa netiboli na michezo kwa ujumla jijini Dar es
Salaam kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuwafahamu viongozi wao, lakini pia
kushuhudia mechi hizo.
No comments:
Post a Comment