MWANAMITINDO Jokate Mwigelo
‘Kidot’ ameona umuhimu wa kuingia kwenye maisha ya ndoa baada ya kuibuka
na kudai kuwa, mwakani na yeye ataolewa.
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
Akizungmza na Ijumaa hivi karibuni kuhusiana na malengo yake kwa
mwaka ujao, Jokate alisema kuwa, miongoni mwa mambo makubwa aliyopanga
kuyatimiza ndani ya mwaka huo ni kuolewa.
“Kikubwa ambacho nafikiria kukitimza mwakani endapo Mungu atanijaalia uzima ni kuolewa ili nami niwe mke wa mtu, atakayenioa kwa sasa ni siri yangu na itakuwa ni ‘sapraizi’ kwa wengi,” alisema Jokate.

Jokate amewahi kuripotiwa kuwa
kwenye uhusiano wa kimapenzi na mcheza mpira wa kikapu, Hasheem Thabit
na pia ikavuma kuwa ametoka na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ ila
mpaka sasa haijulikani kajiweka kwa nani kutokana na mdada huyu kuwa
msiri sana.
HABARI NA Na Hamida Hassan-www.globalpublishers.info
HABARI NA Na Hamida Hassan-www.globalpublishers.info

No comments:
Post a Comment