Na Gladness Mallya
SIKU
chache kabla ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya ndoa yao, wasanii
wa filamu Michael Sangu ‘Mike’ na mkewe Ndumbangwe Misayo ‘Thea’
wamejikuta wakipoteza pete zao kimiujiza.
Michael Sangu ‘Mike’ na mkewe Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao.
Akizungumza kwa huzuni Mike alisema kuwa, yeye na mkewe Thea
walitarajia kufanya sherehe hiyo Novemba 6, mwaka huu lakini hawakuweza
kutokana na siku mbili kabla pete zao za ndoa kupotea katika mazingira
ya kutatanisha.“Yaani tumeshindwa kusherehekea miaka miwili ya ndoa yetu kwa sababu pete zimepotea kwenye mazingira ya ajabu sana. Zote zimepotelea bafuni, tena katika mazingira ambayo hatuyaelewi kabisa.
Mike na Thea wakiwa na pete zao za ndoa zilizopotea katika mazingira ya kutatanisha.
“Tulichokifanya tumeenda kuchongesha pete nyingine na baada ya hapo
tutazipeleka kwa mchungaji akaziombee kabla ya kufanya sherehe hiyo,
tunajua haya ni majaribu ya shetani tu,” alisema Mike.CHANZO CHA HABARI NI GLOBAL PUBLISHERS.

No comments:
Post a Comment