Shakoor Jongo na Musa Mateja - Chanzo cha habari na www.globalpublishers.infoMKATA mayenu wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Grace Utete ‘Kiza Kinene’ juzikati alianza maandalizi ya kufunga mwaka vibaya baada ya kupewa talaka mbili na mumewe aliyetambuliwa kwa jina moja la Abeid.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mapaparazi wetu, lilijiri mchana kweupe
katika Baa ya Ben Kinyaiya iliyopo Kinondoni, Dar huku mkurugenzi wa
bendi anayowajibika mnenguaji huyo, Asha Baraka na meneja wake, Khamis
Kayumbu ‘Amigolas’ wakishuhudia.
Baada ya mnenguaji huyo kupokea talaka, Ijumaa Wikienda lilimvaa na kumuuliza kulikoni kupewa talaka baa, tena mbele ya viongozi wake ambapo bila hata kupepesa macho alijibu kuwa haoni tatizo na kwamba anaifurahia hali hiyo.
Hadi Ijumaa Wikienda linaondoka eneo la tukio, Asha Baraka alikuwa amekaa kikao na aliyekuwa mume wa mnenguaji huyo lakini haikujulikana kikao hicho kilihusu nini.

No comments:
Post a Comment