
Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto.

Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya serikali ya kujenga nyumba mpya 35 kwa ajili ya waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume, amejengewa nyumba ya vyumba vitano pamoja na fremu ya duka.

Pichani
juu na chini ni Baadhi ya nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea
waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma,
Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekana leo Desemba 13, 2012 baada ya
kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.(PICHA NA IKULU).



nyie semeni yote lakini huyu jamaa anapinga kazi bwana .big up mr president
ReplyDelete