ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG),
Barnabas
Mtokambali, amekemea vitendo vya baadhi ya wanaume wanaovaa suruali
chini ya makalio, akisema wanaofanya hivyo ni sawa na mashoga.
Alisema mwanamume kuvalia suruali chini ya makalio ni sawa na
kujitangazia biashara ya ushoga ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Mtokambali alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua Chuo cha Ualimu cha
Mount Sinai kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kama ilivyokuwa kwa machangudoa ambao huvaa nusu uchi kuonesha
kuwa wapo katika biashara, ndivyo hivyo kwa mashoga nao wanavaa ili
kujitambulisha.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo, aliwaasa wanafunzi wa chuo
hicho kuvaa kwa kuzingatia maadili ili wawe walimu bora kwa taifa na
mfano wa kuigwa.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Alexander Chuwa, alisema licha ya chuo
hicho kutoa mafunzo ya ualimu, pia kinatoa mafunzo ya elimu ya biashara
na malengo ya baadaye ni kuwa chuo kikuu.
No comments:
Post a Comment