![](http://api.ning.com:80/files/z5dymxnhcAM2pQp2semqLkU6HBnAervJDA6Sf*ES4FTXMKSkIcGAvLDVQ1Rv04WAhnba9UAFCbT*80BeZ5I-N9BnF3c0hZCr/mastaakilio.jpg?width=650)
VILIO vimetawala katika kaburi la staa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ baada ya baadhi ya mastaa kushindwa kujizuia na kumwaga machozi kutokana na kukumbwa na simanzi.
![](http://api.ning.com:80/files/c80RyWgrPLOjeEUwy7JrwFDqNfw9ZBgaQUnW*hglEhC0qKsuu7WdgSJG0S9tVRn1V4LyYgjOt5JZB*ApEoJKt7n8mAXGohFy/BIRTHDAYKANUMBA4.jpg?width=650)
![](http://api.ning.com:80/files/gQqqlj*uUXoktuvnxIz5ZJ4GTP*fWY6n2gOq-Q-QzA0jg0fCov570EayD372vJRBjtwAd8I-xHZtNGrjd-412mvCA-zFxL*l/BIRTHDAYKANUMBA2.jpg?width=650)
Wasanii walioongoza kumwaga machozi ni pamoja na Blandina Chagula ‘Johari’ na Mayasa Mrisho ‘Maya’ ambao waliungana na marafiki na wana familia kumkumbuka staa huyo kwa kuweka maua, kadi na kuwasha mishumaa kaburini na kumuombea kwa Mungu.
![](http://api.ning.com:80/files/vhkkuu3WVfODtohLkXoEqM27b-4LsDF5PmavCe8RkeFteGPsv6*PwQx8GbJ2-LTw1*YQTkaHeFaKcBORgZlWayTfQoUz4aC5/BIRTHDAYKANUMBA3.jpg)
Baada ya kutoka makaburini waombolezaji hao walikwenda katika Kituo cha Watato Yatima cha CHAKUWAMA kama alivyokuwa akifanya Kanumba kila mwaka katika siku yake ya kuzaliwa.
Katika kituo hicho kilichopo Sinza jijini Dar, wasanii, wanandugu na marafiki waliungana na watoto yatima na kuwapatia chakula pamoja na mahitaji mengine.
![](http://api.ning.com:80/files/A6KI6uJWmu3q2w40Fwv0ejgOTvMXm2WvUQpT9ikuWt5KTLKMnXn7p-ByGHd2qhMbmQ6v8FPzw9Ykq53Jdsh40I8AYrt4Cm4N/BIRTHDAYKANUMBA1.jpg?width=650)
Akizungumza na Ijumaa mdogo wa marehemu, Seth Bosco alisema ataendelea kumkumbuka Kanumba na kufanya kila jema alilokuwa akilifanya.
Mbali na Johari na Maya, Chopa Mchopanga na Kadadaa walioshiriki, wasanii wengine wa filamu walikacha kuungana na familia kumuenzi Kanumba katika siku yake hiyo ya kuzaliwa huku mama mzazi wa marehamu, Flora Mtegoa akiwa Bukoba akimuuguza mama yake.
![](http://api.ning.com:80/files/z5dymxnhcAORtWwyK6TzUOGdmoDKOyoYC9enGFQzKRdyv4DD9Jd*a78c0WJzyKLERbxLZM-LpEl9g2tphYhhOtFUrCuvIULk/BIRTHDAYKANUMBA5.jpg?width=650)
CHANZO CHA HABARI NI GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment