HALI ya mke wa Marehemu Sajuki, Wastara Juma ni ya kusikitisha na inahitaji moyo mgumu kukaa nae na kumfariji.
Wastara
alipitisha siku nzima ya jana akilia bila kupumzika, karibu kila msanii
aliyeingia chumbani mwake kwenda kumsalimia alikutana na kilio cha
Wastara.
Mh. January Makamba akijaribu kumfariji Wastara
Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba nae akimfariji Wastara
Hali
hiyo ilipelekea baadhi ya wasanii kuhofia kwenda kumsalimia kwa kuamini
kuwa watakuwa wanaenda kumliza upya badala ya kumfariji.
Saluti5
ilipojaribu kuingia chumbani kwa Wastara ikiwa imeongozana na wasanii
Mrisho Mpoto, Issa Mussa “Cloud” na Lumole Matovolwa “Big” ilikutana na
kilio kizito na hakuna aliyethubutu kupoteza hata dakika mbili chumbani
humo.
Jaqline Wolper, mmoja kati ya watu waliotoa mchango mkubwa wakati wa kumuuguza Sajuki
Mohamed Said, mdogo wa marehemu, ambaye ndiye aliyekuwa akimuuguza Sajuki hospitalini hadi kifo chake
Historia
ya wasanii hao wawili (Sajuki na Wastara) iliyopitia misukosuko na
mitihani mikubwa, inafichua penzi zito na la kweli miongoni mwao, hali
ambayo itamfanya Wastara asikaukwe na chozi kwa muda mrefu wa maisha
yake.
Zamaradi Mketema wa Clouds TV (mwenye begi katikati) akiwa na waombolezaji wengine jana nyumbani kwa marehemu Sajuki
Umati uliofurika kumboleza msiba wa Sajuki
Sajuki
alifariki jana alfajiri kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
anatarajiwa kuzikwa kesho mchana kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment