MSANII
 maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana 
leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.
Dhamana
 hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es 
Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti
 aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali
 wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya 
kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo 
itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.
 
 
 
 
 
 
 

 
No comments:
Post a Comment