EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, January 28, 2013

Mwakyembe: Bandari ya Dar kuwa ya mfano kwa ubora

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameeleza nia yake ya kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya mfano duniani kwa utoaji wa huduma bora za upakiaji na upakuaji kwa wananchi wa ndani na nje ya nchi.
 
 WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe. 
Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na madereva wa malori na wadau wengine wa bandari baada ya madereva hao kumtaka awasikilize kero zao wakati alipokuwa bandarini hapo na msafara wa mawaziri kutoka nchini Uganda.
Dk Mwakyembe alilazimika kurudi bandarini hapo jana baada ya juzi kuombwa na madereva hao kuonana naye ili wamweleze kero zao na yeye aliahidi kurudi kesho yake ambayo ilikuwa jana.
Katika mazungumzo hayo Waziri Mwakyembe aliwataka madereva hao kuwa wawazi kueleza kero zote zinazowakabili bandarini hapo kwa kuwa yeye hasa ndiye mwenye dhamana ya kurekebisha na kuboresha huduma bandarini.
Wadau hao walimweleza waziri kuwa kero ni nyingi zikiwamo za upatikanaji wa vibali vya upakiaji na foleni ya magari, ratiba na muda wa kupakia, mwingiliano wa kazi za meli na malori ya mizigo na madai ya rushwa kwa wafanyakazi hasa wa kitengo cha upakiaji wa makontena bandarini hapo.

Waziri aliwataka watendaji bandarini hapo kuondoa urasimu kwani hakuna haja ya malori ya kusafirisha mizigo nje ya nchi kuwa na foleni ndefu bandarini hapo kwa kuwa suala hili linapunguza ushindani wetu katika soko.

“Hakuna haja ya malori ya mizigo yaendayo nje ya nchi kuchelewa kutoka, na ndiyo sababu inayofanya Mombasa wanatuzidi kwa ufanisi” alisema Mwakyembe.
Katika kuimarisha utoaji wa huduma waziri aliwataka TICTS kufanya kazi kwa saa 24 kila siku na kwa siku saba ili kuondoa msongamano wa malori tofauti na sasa ambapo mizigo hupakiwa siku za Jumatatu mpaka Jumatano kuanzia saa 5.00 asubuhi kwa awamu tatu kwa siku kama alivyothibitishiwa na Meneja wa TICTS Bandari ya Dar es Salaam, Daniel Tawale. 

Akitafuta suluhu ya kero zote za bandarini hapo toka kwa wadau tofauti, waziri alisema kuwa kamati ya muda iundwe ili kwa muda wa siku saba ifanye utafiti na imshauri nini cha kufanya ili kuinusuru bandari hiyo.
“Nataka niunde kamati ndogo sasa hivi ili ichunguze na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike na inipe majibu ndani ya siku saba ofisini kwangu ili niweze kufanya uamuzi sahihi kwa kuwa ni lazima tubadilike ili tuweze kuhudumia wateja wengi wanaotuzunguka” alisema waziri wakati akiunda kamati hiyo.

Waziri aliunda kamati ndogo yenye wajumbe 10 toka sekta tofauti za wadau wa bandari ambayo itaongozwa na Daniel Silla toka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili kuchunguza na kubainisha kero zilizopo bandarini hapo na suluhisho zake.
Wajumbe wengine walioteuliwa ni sekta zao kwenye mabano ni Castrol Felician (TRA), Meshack Gideon (Dereva wa Ndani), Chacha Lukwi (Mshauri wa Madereva), Agness Mathias (KK Security), John Masasi (TICTS), William Kapera (TPA Usalama), Martin Paul (Evergreen Shipping Agent), Jones Jonathan (Wakala Usafirishaji) na Aloyce Gabriel (Wakala Uingizaji).
“Tarehe 03 mwezi Februari nataka ripoti ofisini kwangu ikiwa na uchunguzi mlioufanya ili kuiboresha bandari hii kwa kuwa nataka tuwe bandari ya mfano katika dunia hii” alisema Dk Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate