
Kwa mujibu wa maafisa wa afya, wawili hao walipigwa risasi wakiwa kando ya medani ya 
Tahrir.Ripoti zinasema kuwa mwanamume mmoja alifariki katika eneo la Tahrir wakati wa pili alifariki hospitalini.
Tahrir.Ripoti zinasema kuwa mwanamume mmoja alifariki katika eneo la Tahrir wakati wa pili alifariki hospitalini.
Zaidi ya watu 50 wamefariki katika makabilino katika baadhi ya miji nchini misri katika wiki moja iliyopita.Hizi ghasia zimesemekana kuwa mbaya zaidi tangu rais Morsi kungia mamlakani.Wakosoaji wanamtuhumu kwa kuhujumu faida za mapinduzi ra kiraia.
Rais Mursi ameenda mjini Berlin Ujerumani kuomba
 mkopo unaohitajika sana licha ya ghasia, zinazoendelea kwa sikub ya 
saba mjini Cairo.
Serikali ya Morsi iko kwenye mazungumzo na 
shirika la fedha duniani kuhusu mkopo wa dola bilioni 4 nukta nane 
lakini makubaliano ya mwanzo kuhusu mkopo huu yalijikokota kwa sababu ya
 hofu kuwa mgogoro wa kisiasa unaoshuhudiwa Misri kwa sasa huenda 
ukahujumu mageuzi ya kifedha.
Bwana Morsi atajaribu kumshawishi chansela wa 
ujerumani, Angela Merkel kuwa serikali yake ingali inasisitiza kuwa 
demokrasia sharti, itazingatiwa.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa hii ni ishara ya 
maswala ya kifedha ya nje yalivyo ni muhimu kwa Misri na ndiposa rais 
Morsi akaamua kufanya safarai nje wakati nchi inatokota.
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment