Mwili wa raia wa Ghana
aliyekuwa anafanya kazi ya uvuvi Ireland Kaskazini , bado uko kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kifo chake.
Juhudi za kutaka kuurejesha mwili wake nyumbani kwao mazishi hadi kufikia sasa hazijafanikiwa.Fortune Adzawoloo, 29, alifariki mwezi Julai mwaka 2011, wiki sita baada ya kuanza kazi yake ya uvuvi.
Familia yake, inataka mwili wake kurejeshwa nyumbani lakini wanazozana kuhusu nani atagharamia safari hiyo.
Shirika moja limejotolea kulipia mazishi yake lakini sharti yafanyike nchini humo lakini jamaa zake wamekataa pendekezo hilo.
Kulingana na mwakili wa kisheria wa familia hiyo, marehemu alikuwa chifu katika jamii yake nchini Ghana.
Tamaduni za watu wa Ghana zinasema kuwa anapaswa kuzikwa mahala maalum nyumbani kwao.
No comments:
Post a Comment