Na Mwandishi Wetu
MZEE mmoja, Petro Keiya Mdee anayetibiwa katika Hospitali ya KCMC akisumbuliwa na maradhi ya miguu, amekatwa miguu mara mbili ndani ya wiki mbili, hivyo sasa kulazimika kuomba jamii imsaidie.
Petro Keiya Mdee.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa Uchiro Moshi, mzee huyo alisema:
“Nilianza kuumwa miguu mwezi wa nane mwaka jana. Nilianza kusikia ganzi miguuni, ikaanza kuvimba na baadaye malengelenge yakanitoka yakawa yanatoa harufu mbaya.
“Nimekuwa nikitibiwa hapa KCMC sasa hali ilipozidi kuwa mbaya Novemba 29, mwaka jana nikaambiwa ni lazima miguu ikatwe chini ya magoti, sikuwa na lakufanya nikakubali, ikakatwa.
“Lakini hali haikubadilika kwani madaktari walipoangalia wakasema inabidi ikatwe tena juu ya magoti na Desemba 12, mwaka jana, ikakatwa.
“Sijapata nafuu, bado naumwa sana, nateseka, nimetokwa na kidonda mgongoni kutokana na kushindwa kuketi au kujigeuza.
“Hivi sasa nimerudi nyumbani Uchiro Moshi ambako naugulia lakini sina chochote cha kunisaidia, naomba yeyote aliyeguswa na tatizo langu anisaidie kwa kutumia namba 0712490245 au 0766025351,” alisema kwa masikitiko mzee huyo.
CHANZO CHA HABARI NA GROBALPUBLISHERS

No comments:
Post a Comment