Picha juu na chini ni Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency
wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za
Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni
utaratibu wa hoteli hiyo kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili
kutunza mazingira.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya
usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar
zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo
iliyojipangia kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza
mazingira.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro Ltd Bw. Abdallah
Mbena (kushoto) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika fukwe za
Kivukoni Front baada ya kupata mwaliko kutoka Hoteli ya Hyatt Regency wa
kushiriki katika kusafisha fukwe hizo.
Mwananchi asiyefahamika akiwa amechapa usingizi huku akiwa amejifunika
gunia chafu na kulifanya kuwa shuka katika kichaka cha fukwe za Kivukoni
Front wakati zoezi la usafi likiendelea.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency
Kilimanjaro wakiwa wamebeba mafurushi ya lundo la uchafu uliokusanywa
kutoka kwenye fukwe za Kivukoni Front zilizopo karibu na Hoteli hiyo.
Moja ya magari ya kukusanya uchafu ya kampuni ya Green Waste Pro likiwa
limesheheni lundo la uchafu uliokusanywa toka kwenye Fukwe za Kivukoni
Front baada ya kusafishwa na Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa
kushirikiana na kampuni ya usafi ya Green Waste Pro.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency na wafanyakazi wa kampuni ya
usafi ya Green Waste Pro ltd wakibadilishana mawazo baada ya kuhitimisha
zoezi la kusafisha fukwe za Kivukoni Front na kuishukuru kampuni ya
Green Waste Pro kwa kuitikia wito.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Hyatt Regency na kampuni ya Green Waste Pro baada ya zoezi la usafi.
No comments:
Post a Comment