Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,
WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,mara baada ya makabidhiano ya msaada wa
vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom
Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo Nyamisati iliyopo wilaya Rufiji
Mkoa wa Pwani.
Rufiji-Pwani
-- Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, mama Salma Kikwete, amekabidhi
msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20,
kwenye Kituo cha Afya cha Nyamsati, mkoani Pwani, uliotolewana Mfuko wa
Huduma za Jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Hafla ya
makabidhiano hayo imefanyika leo, katika Kituo cha Afya cha Nyamsati
mkoani hapa, ambapo pamoja na mambo mengine, mama Kikwete ameishukuru
Vodacom Foundation kwa msaada huo, nakutoa rai kwa wadau wengine
kujitokeza na kuunganisha Nguvu katika kukabiliana na matatizo ya
kijamii, hasa eneo la afya ya mama na mtoto.
"Idadi ya vifo vya mama na mtoto, mapambano dhidi ya Malaria na UKIMWI, chanjo kwa watoto ikiwemo ya ugonjwa wa Nimonia, mimba kwawanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha wajasiriamaliwa kike ni mambo muhimu ambayo jamii inapaswa kuyatazama kama changamoto na kuangalia namna ya kukabiliana nayo," amesema.
Mama Kikwete amesema upungufu wadawa na vifaa tiba kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini bado ni changamoto, na kwamba msaada uliotolewa utasaidia kuunga mkono jitihada za Serikali zenye lengo la kuleta ustawi wa huduma za Afya kwa manufaa ya watu wa Nyamsati na mkoa wa Pwani kwa ujumla.
Akipokea msaada huo, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyamsati wilaya ya rufiji mkoa wa pwani Bw.Haruna Mhina alisema Kituo hicho cha afya ambacho kinahudumia wastani ya wagonjwa 2000 kwa mwezi kinakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madawa na vifaa tiba lakini kupitia msaada huo, kwa kiasi kikubwa utasaidia kutatua ukubwa watatizo hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mfuko wa Kusaidia Jamii wa Vodacom,Bw. Yessaya Mwakifulefule, amesema kuwa mfuko huo siku zote umekuwa mstari wa mbele kushirikiana na taasisi na vituo kadhaa vya afya nchini katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini kupitia misaada mbalimbali wanayoitoa.
"Azma ya Vodacom nikuhakikisha tunaifikia jamii na kushirikiana nayo katika kukabiliana na changamoto zinazoizunguka kwenye maeneo yote,hususani afya na elimu, na tutaendelea kuisaidia Nyamsati kadiri itakavyowezekana ili kuleta ustawi mzuri kwa afya ya watu wake," amesema Mwakifulefule.

WAMA,Mama Salma Kikwete(katikati) pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya
Nyamisati, iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani Bw.Haruna Mhina,wakipokea
msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20
kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
No comments:
Post a Comment