Wakenya
watakaopokea rushwa kutoka kwa wanasiasa ili kuwapigia kura wakati wa
uchaguzi mkuu mwezi Machi huenda wakajipata matatani.
Kulingana na nakala ya sheria zilizotolewa na
tume huru ya uchaguzi na mipaka , mtu yeyote atakayepokea pesa au
chakula ili kumuunga mkono mgombea fulani, atakuwa anakiuka sheria za
tume hiyo.

Wapiga kura wakijisaji
Pia mpiga kura atakuwa anakiuka
sheria kwa kupokea chakula , kinywaji , pesa au vyeti kwa lengo la
kushawishiwa kumpigia kura mgombea fulani, huenda akakamatwa.
Kulingana na nakala ya sheria za tume hiyo
kuhusu uchaguz, maafisa maalum wa polisi watatateuliwa kutoa usalama
wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Machi.
Pia nakala hiyo inaelezea kuwa mgombea yopyte
atakayetumia rasilimali za serikali kuwalazimisha wapiga kura kuwaunga
wagombea fulani au chama fulani cha kisiasa.
Washukiwa wa vitendo hivyo watafikishwa
mahakamani huku mkuu wa polisi akisema kesi kama hizo zitachukua miaka
mitatu kabla ya hukumu kutolewa.
Yeyote atakayepatikana na hatia huenda akafungwa
jela miaka sita au kutozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za
Kenya. Nchini Kenya ni jambo la kawaida kwa wanasiasa kuwashawishi
wapiga kura kwa pesa au chakula ili waweze kuwapigia kura.
No comments:
Post a Comment