
BENDI
ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma “ Ijumaa hii watatambulisha nyimbo
zao mpya katika ukumbi wa Masae Garden View uliopo Kawe.Akiongea msemaji wa kundi hilo, Kelvin Mkinga amesema katika onyesho
hilo bendi yake itatambulisha ‘silaha’ zao zote zitakazokuwemo katika
albam yao mpya itakayojulikana kama “Chuki ya nini” ambayo itazinduliwa
baadae mwaka huu.
Aidha, Kelvin amesema mbali na nyimbo mpya, pia watashusha rap zao mpya ikiwemo ile ya Ugali kwa kachumbari.
Habari na saluti5
No comments:
Post a Comment