Kiongozi nambari 3 wa kundi la waasi wa Answaruddin la kaskazini
mwa Mali amekamatwa karibu na mpaka wa Algeria alipokuwa akikimbia
mashambulizi ya vikosi vya jeshi la Ufaransa.
Muhammad Moussa amepelekwa katika mji wa Kidal uliokuwa ngome ya
mwisho ya waasi wa Mali, walikofurushwa katika mashambulizi ya vikosi
vya nchi hiyo vikisaidiwa na askari wa Ufaransa.
Taarifa za kukamatwa
kiongozi huyo wa waasi zimethibitishwa na Abdoulaye Toure, afisa wa
serikali ya Mali katika eneo la Kidal aliyesema kuwa, kiongozi huyo wa
waasi amekamatwa na kundi jingine hasimu la waasi wa kaskazini mwa Mali
la Tuareg.
Wakati hayo yakiripotiwa ndege za vita za Ufaransa zimeendelea
kushambulia kambi za waasi karibu na mji wa kaskazini mwa Mali wa
Tessalit, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Algeria. Thierry Burkhard
msemaji wa jeshi la Ufaransa amesema, mashambulizi hayo yalianza jana
usiku na yamelenga maeneo muhimu na kambi za mafunzo zilizoripotiwa
kutumiwa na wapiganaji wa kundi la al Qaida.
No comments:
Post a Comment