Jumlaya
magunia 20 ya madawa ya kulevya aina ya bangi yanayokadiriwa kuwa na
uzito wa kilogramu 50 kila moja yamekatwa na askari wa Jeshi la Polisi
Mkoani hapa. Tukio hilo lilitokea tarehe 31/01/2013 muda wa saa 7:30
usiku katika kitongoji cha Losoiti kijiji cha Kimokuwa wilayani Longido.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna
Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas alisema kwamba mafanikio hayo
yametokana na ushirikiano mzuri kati ya Jeshi hilo na wananchi ambapo
baadhi ya raia wema walitoa taarifa kwa jeshi hilo kuhusiana na kuwepo
tukio hilo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna
Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas alisema kwamba mafanikio hayo
yametokana na ushirikiano mzuri kati ya Jeshi hilo na wananchi ambapo
baadhi ya raia wema walitoa taarifa kwa jeshi hilo kuhusiana na kuwepo
tukio hilo.
Kamanda
Sabas alisema kwamba, katika tukio hilo mtu mmoja mwanaume
aliyejulikana kwa jina la Mandege Pakasi (54) Mfugaji na ni mkazi wa
Longido amekamatwa huku wenzake wawili wakifanikiwa kukimbia.
Alisema
kwamba watu hao walikuwa wanasafirisha magunia hayo kutoka eneo hilo
kwenda nchi jirani ya Kenya kwa kutumia wanyama aina ya Punda ambapo
jumla ya Punda 10 walitumika na kila punda alibeba magunia mawili.
Jeshi
la Polisi Mkoani hapa bado linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo huku
watuhumiwa wengine wakiendelea kutafutwa. Kufuatia mafanikio hayo
Kamanda huyo amewashukuru wakazi wa Mkoa huu kwa ushirikiano wanaoutoa
kwa jeshi hilo na ameendelea kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano katika
kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
Ukiachana
na tukio hili kwa mwaka huu 2013 jeshi hilo mkoani hapa limekamata
magari mawili yakiwa na jumla ya viroba 374 vya madawa ya kulevya aina
ya mirungi kwa nyakati tofauti huku kesi za matukio hayo zikiwa tayari
zimekwishafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment