Rais wa Ufaransa, Francois
Hollande, amewasili mjini Timbuktu, Mali, ambao wanajeshi wa Ufaransa na
Mali waliukomboa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu siku sita
zilizopita.

Mwandishi wa BBC huko anasema Bwana
Hollande amepokelewa kwa shangwe kwa sababu watu wa Timbuktu wamepumua
kuwa utawala wa kikatili umemalizika.
Kiongozi huyo wa Ufaransa - akifuatana na
mawaziri kadha - anafanya ziara ya siku moja nchini Mali ili kuwaunga
mkono wanajeshi wake.
Akizungumza mjini Paris kabla ya kuondoka, Bwana Hollande alieleza azma ya safari yake:
"Nakwenda Mali kuwaambia wanajeshi wetu jinsi tunavyowaunga mkono na kuwapa moyo na kwamba tunawaonea fahari.
Nakwenda Mali kuwezesha majeshi ya Afrika
yajiunge nasi haraka iwezekanavyo, na kuwaambia kwamba tunawahitaji kuwa
sehemu ya kikosi cha kimataifa.
Piya nakwenda Mali kuhakikisha kwamba kutakuwa
na mazungumzo ya kisiasa - kwa vile sasa imewakimbiza wapiganaji -
mazungumzo ya kutafuta utulivu na mkataba wa amani."
No comments:
Post a Comment