EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, March 3, 2013

Aliyeisababisha TPA hasara ya mabilioni akingiwa kifua

Menejimenti na Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) imeshikwa kigugumizi kumweka wazi mtu aliyehusika kubadilisha kipengele cha mkataba wa ujenzi wa Mtambo wa Kupakua Mafuta kwenye Meli (SPM) bandarini na kusababisha hasara ya dola za Marekani 3 milioni  karibu sawa na Sh4.8 bilioni.
 
Kutokana na kubadilishwa kwa kipengele hicho, TPA italazimika kutoa kiasi hicho cha fedha katika kipindi cha miaka miwili kwa ajili ya kukarabati mtambo huo ambao tayari umeanza kufanya kazi miezi sita iliyopita.

Siri ya kuondolewa kwa kipengele hicho iliwekwa hadharani Januari 18 mwaka huu na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe alipofanya ziara fupi bandarini sambamba na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoba na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

Kipengele hicho kinaeleza kwamba, mara baada ya mwekezaji  aliyejenga mtambo huo ambaye ni Kampuni ya Leighton ya Singapore atakapokamilisha ujenzi, angeiachia TPA vifaa vya ukarabati wa mtambo huo vyenye thamani ya Sh4.8bilioni.


Lakini baada ya mwekezaji huyo kukabidhi mtambo huo ilibainika kuwa kipengele hicho kimeondolewa hivyo kulisababishia Taifa hasara.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zilieleza kwamba kukosekana kwa vifaa hivyo kutasababisha hasara na usumbufu mkubwa kwa kukwamisha shughuli za upakuaji wa mafuta kwa kiwango cha juu.

“Kama mtambo utaharibika ni wazi kuwa hakutakuwa na vipuri… Lakini kama ikilazimu hivyo TPA itaingia gharama ya kununua vipuri hivyo wakati mkataba ulieleza kuwa spea hizo zitatolewa na mkandarasi,” Kilieleza chanzo cha habari hizi.
Katika mkutano huo wa Januari 18, mwaka huu, Dk Mwakyembe alitoa siku tatu ili apatiwe majibu ya kasoro zilizojitokeza.

Mpaka sasa Menejimenti na Bodi ya TPA wamekuwa wakigoma kuzungumzia suala hilo wakisema mwenye mamlaka ya kulizungumzia ni Waziri.
Hata hivyo, Dk Mwakyembe naye alikataa kuzungumzia juu ya utekelezwaji wa maagizo yake akilitaka Mwananchi Jumapili kuwasiliana na menejimenti.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya TPA, Julius Mamiro aligoma kueleza hali iliyopo sasa na kutaka atafutwe Mwenyekiti wake, Profesa Joseph Msambichaka.
Profesa Msambichaka alipoulizwa alisema kuwa masuala yote ya Mamlaka hiyo yanatolewa ufafanuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Madeni Kipande.

“Siwezi kuzungumza mpaka nipate ruhusa kutoka kwake kwa sababu hatuwezi wote kuwa wazungumzaji,” alisema Profesa Msambichaka.
Mweananchi Jumapili lilipowasiliana na  Dk Mwakyembe alisema kuwa maelezo ya kina yanaweza kutolewa na Menejimenti na  bosi ya TPA.
“Wakati mwingine sio vyema kuwajibia maswali watu wa TPA. Hebu watafute uwaulize wao ndiyo wana majibu sahihi” alisema Dk Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate