SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza Polisi,wakuu
wa mikoa na wilaya kutofanya ajizi kwenye suala la wachochezi wa kidini ,
badala yake wachukue hatua stahiki,baadhi ya wasomi na wanaharakati
wamepinga kauli hiyo na kudai ni maneno ya kisiasa.
Wamedai kuwa kuanzia Serikali ya Awamu ya Tatu hadi hii ya nne zimekuwepo kauli za kupiga marufuku kashfa dhidi ya dini nyingine lakini kukashifiana kumekuwa kukifanyika tena kwa uwazi bila hatua kuchukuliwa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk
Benson Bana amesema kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni kauli ya kisiasa na
alitakiwa kutoa tamko la kuwawajibisha watendaji wake pindi
wanaposhindwa kutekeleza wajibu wao.
Alisema vitendo hivi vyote vya machafuko ya
kidini vinafanyika hadharani huku wakuu wa mikoa,wilaya na Usalama wa
taifa wakishuhudia wakati jukumu la kulinda amani katika eneo husika ni
lao.
Naye Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama Cha Wananchi
(CUF), Julius Mtatiro anasema Serikali inayoongozwa na CCM haina uwezo
wa kutokomeza udini.
Katika hotuba yake ya kawaida ya kila mwisho wa
mwezi aliyoitoa Februari 28, mwaka huu, Rais Kikwete aliiagiza Polisi
nchini kukamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na
wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa
wengine.
Aliwataka wakuu wa mikoa nao kutoona ajizi katika hilo.
No comments:
Post a Comment