
UNNA, UJERUMANI- Habari na Saluti5.com
MWANAMKE
mmoja nchini hapa, Karin Hoffer amepandishwa kizimbani akidaiwa kutaka
kumuua mpenzi wake kwa kumziba pumzi na maziwa yake.
Karin anatuhumia kwa kumlazimisha mpenzi wake huyo kuingiza kichwa katikati ya maziwa yake wakati wakifanya mapenzi.
Mahakama
ilielezwa kwamba mpenzi wake huyo, Andreas Koller alihangaika kupumua
wakati alipokuwa amebanwa kisawasawa na mwanamke huyo.
Waendesha
mashitaka wamesema kuwa wakati Andreas alipojaribu kupumzika kwa
kuondoka kifuani, Karin mwenye umri wa miaka 33, alimvuta na kumbana kwa
mikono yake.
Majaji
waliahirisha kesi hiyo baada ya wanasheria wa upande wa utetezi
kuiambia mahakama kuwa mtuhumiwa anasumbuliwa na matatizo ya
kisaikolojia na asingeweza kupanda kizimbani.
Andreas
aliiambia mahakama: “Hakika nilimpenda kwa moyo wangu wote, lakini
ninachohitaji si maneno, bali kufanyika uchunguzi kuthibitisha kama ana
akili sawasawa ama la.”
No comments:
Post a Comment