EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, March 2, 2013

Benki hazijajipanga kudhibiti wizi ATM

SASA ni dhahiri kwamba benki zetu hapa nchini zimezidiwa nguvu na mitandao ya wizi wa fedha kupitia mashine za kutolea fedha (ATM). Vyombo vya habari vimekuwa vikitoa habari za wizi huo kila kukicha, huku benki hizo zikihaha kuficha habari hizo kwa hofu ya kukimbiwa na wateja.

Baadhi ya benki zimekiri kwamba tatizo la wizi wa fedha kutoka katika akaunti za wateja sasa limezizidi kimo, kwa maana ya kuota mizizi na kuwanyima usingizi watendaji wa benki hizo.
Pamoja na juhudi za benki hizo kujaribu kupata suluhisho la pamoja kuhusu wizi huo, mtandao huo wa wizi umekwamisha juhudi hizo kutokana na kubuni mbinu mpya siku hadi siku.

Maofisa wa benki pia wameshtushwa na kiwango kikubwa kinachoibwa hivi sasa, kutoka malaki na mamilioni miaka miwili mitatu iliyopita hadi kufikia mabilioni katika siku za hivi karibuni. Maofisa hao wanakubaliana katika mambo mawili makubwa. Kwanza, kwamba tatizo ni kubwa na liko juu ya uwezo wao. Pili, kwamba mtandao huo mkubwa ni wa kimataifa na unaratibiwa kutoka katika miji mikubwa duniani yenye mashina katika nchi zenye udhibiti legelege wa fedha kama Tanzania.


Hapa Tanzania, hapo mwanzo wizi huo ulikuwa katika Jiji la Dar es Salaam na baadaye benki zikashtukia mtandao huo ukiwa tayari umepanuka hadi miji mikubwa mikoani, kabla haujabisha hodi kwa kasi katika miji midogo iliyoko vijijini.
Hivyo, maofisa wengi wa benki hawalioni tukio la juzi kama la kushangaza, ambapo polisi wilayani Rungwe, mkoani Mbeya waliwanasa watu wanne, akiwamo mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana wakiiba fedha katika ATM ya Benki ya NMB, Tawi la Tukuyu kwa kutumia kadi 150 bandia za ATM.

Tumeambiwa kwamba hadi wanatiwa mbaroni tayari walikuwa na zaidi ya Sh20 milioni kibindoni. Polisi wanasema kadi zote walizokutwa nazo zilikuwa zinaonyesha  ni za walimu kutoka wilayani Mbozi. Swali lililowatatiza maofisa wa benki na vyombo vya usalama ni kwa nini kadi zote hizo za wilayani Mbozi zipelekwe kutolea fedha katika ATM za wilayani Rungwe?

Kama benki sasa zimekiri kwamba hazina uwezo wa kuma liza tatizo hilo, lazima tukubaliane kwamba sasa zinahitajika nguvu na mbinu za ziada. Hatuwezi tena kuziachia benki zetu kupambana kichwakichwa na mitandao ya wizi wa fedha yenye zana na teknolojia ya kisasa, wakati tuki tambua kwamba kufanya hivyo ni kuziharakishia kifo.
Ebu tuangalie wajibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ina wajibu mkubwa wa kusimamia na kuratibu benki zote nchini kisera. 

Hatuoni benki hiyo mama ikifanya juhudi za kutosha kuishauri Serikali kuingilia kati suala la mitandao ya wizi wa fedha za wateja kupitia ATM. BoT inapaswa kutoa miongozo na maelekezo kwa benki hizo kuhusu masuala mbalimbali ya kuhakikisha fedha za wateja wa benki hizo zinakuwa salama.

Hii ni pamoja na kuangalia upya teknolojia inayotumiwa na benki zetu. Yapo madai kwa mba benki hizo zinatumia mashine chakavu za ATM ambazo ni mitumba kutoka nchi za nje. Madai mengine ni kwamba baadhi ya mafundi wa mashine hizo ndiyo wanashirikiana na mitandao ya wizi ndani ya benki zenyewe kuwaibia wateja.
Hata hivyo, yote hayo yanatokea kwa sababu vyombo vyetu vya usalama vimelala usingizi wa pono na vinasubiri tu kuzinduliwa na raia wema ndipo vichukue hatua. Tunadhani umefika wakati wa kuviwajibisha ili vijihusishe tu na kazi vilivyoanzishwa kuzifanya.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate