Dar es Salaam. Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam (Udasa), imesema hakuna haja ya wanasiasa kufanya maandamano ya
kupinga matokeo mabaya ya kidato cha nne na badala yake wanatakiwa
kushirikiana na Watanzania kudai mfumo mpya wa elimu.
Mbali na hilo, wamesema kwa sasa wanatakiwa kusubiri majibu ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufuatilia chanzo cha wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani yao ili wajue tatizo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa
Jumuia hiyo, Dk Francis Michael wakati akitoa taarifa ya kukemea
vitendo mbalimbali vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi ya
watu.
No comments:
Post a Comment