Malkia Elizabeth wa Uingereza amelazwa
hospitali mjini London akiwa anaugua tumbo. Alipelekwa hospitalini
mwishoni mwa juma lililopita.
Taarifa kutoka makao yake ya Kasri la Buckingham
zinasema kuwa shughuli zote rasmi za malkia zimeahirishwa ama kufutwa,
ikiwa ni pamoja na ziara aliyotarajia kufanya mjini Roma.

Malkia Elizabeth, mwenye umri wa miaka 86,
alipelekwa hospitali ya King Edward VII baada ya kuonyesha dalili za
‘gastroenteritis’, Kasri la Buckingham lilisema. ‘Gastroenteritis’
husababisha uvimbe tumboni.
Kasri la Buckingham lilisema kwamba hali ya
malkia ilikuwa siyo mbaya, na kwamba alikuwa hajalala kitandani, bali
alikuwa anatembeatembea.
Hii ni mara yake ya kwanza kulazwa kwa muda wa
miaka 10 iliyopita, na inategemewa kwamba atabaki hospitali kwa
uchunguzi kwa siku mbili zijazo.
No comments:
Post a Comment