EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, March 28, 2013

Mbunge aanguka kikaoni ni Salim Hemed Khamis (CUF).

MBUNGE wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), jana alianguka ghafla katika mkutano wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Salim alianguka saa tano asubuhi wakati akihudhuria mkutano wa kamati hiyo, uliokuwa ukifanyika katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilizua hofu kwa wabunge wengine waliokuwamo, ambapo mkutano huo ulisitishwa kwa muda na juhudi za kumshughulikia zilianza, kwani alitolewa nje ya ukumbi na kuanza kupepewa.

Hata hivyo mbunge huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuingizwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa, alilazimika kutoka nje ya ukumbi ambapo aliungana na wenzake katika kuchanga mawazo kuhusu namna ya kumpeleka hospitali mbunge huyo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, hali ya mbunge huyo anayedaiwa kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu iliendelea kubadilika, huku akitokwa na jasho jingi.

Kutokana na hali hiyo, mwishowe mbunge huyo alipoteza fahamu katika majengo ya Ofisi za Bunge, kitendo ambacho kiliwafanya wabunge wenzake kushindwa la kufanya.

Wabunge wanne walijaribu kumbeba mbunge huyo ili waweze kushuka naye chini, lakini walishindwa kutokana na uzito wake na hivyo wakalazimika kuomba msaada kwa waandishi wa habari.
Hata hivyo Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) aliwashangaza wenzake kutokana na kitendo chake cha kuwazuia waandishi wa habari kupiga picha kwa kuziba kamera zao akitumia makabrasha ya vitabu.

Waandishi wa habari watano walichukua takribani dakika nane kumbeba akiwa kwenye kiti hadi kumpeleka katika gari lenye namba za usajili STK 2178 Land Cruiser na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Nkamia alishangaza tena pale alipoacha kazi ya kusaidia kumbeba mwenzake, badala yake akaenda pembeni na kuanza kuvuta sigara, hali iliyofanya waandishi wabaki kumshangaa.

Akizungumzi tukio hilo, Lowassa hakuweza kueleza mazingira ya kunguka kwake, ingawa alithibitisha kwamba mbunge huyo aliugua ghafla na baadaye alianguka.

“Hivi sasa yupo ICU, kwani baada ya kumfikisha pale Muhimbili walimpeleka katika uangalizi maalum na timu ya madaktari inaendelea kumhudumia, taarifa za maendeleo ya afya yake tutaendelea kuzitoa,” alisema.

Waandishi waliombeba mbunge huyo ni Nuzulack Dausen (Mwananchi), Benjamin Masese (Mtanzania), Muhibu Said (Nipashe), Cosmas Hinju (Radio Uhuru) na Mohamed Issa (Uhuru na Mzalendo).

Mbali ya Nkamia, wabunge wengine waliokuwapo karibu ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mbunge wa Kikwajuni, Hamad Masauni na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF).

Katika hatua nyingine, kabla ya tukio hilo, kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Arusha (AICC) kujadili utendaji wao.

Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilipitia hesabu za kituo hicho, ingawa wajumbe hawakuridhishwa na uwekezaji uliofanywa katika kituo hicho cha kimataifa.

“Tunatarajia kwenda ili kuona hiyo miradi mbalimbali ya kituo, ikiwamo majengo, vituo vingine vya uwekezaji, kwani lengo letu ni kuongeza kasi ya uwekezaji.

“Tunataka watueleza hali halisi ya uwekezaji ili tujue nini kinachowakwamisha washindwe kwenda kasi na badala yake wanaendelea kusuasua,” alisema.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate