Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa
Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta
anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi
hiyo, Raila Odinga.

Kama alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.
Hadi majira haya ya saa 6.45 usiku wa kuamkia leo, Uhuru ambaye ni mgombea wa TNA alikuwa amepata kura 744,648 sawa na asilimia 56.1 wakati Raila ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia kwa kupata kura 527, 780 sawa na asilimia 39.7.
Matokeo hayo ni kutoka katika vituo zaidi ya 5000
kati ya 31,000 na yalikuwa yakionyeshwa moja kwa moja na Tume Huru ya
Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) kadri yalivyokuwa yanaingia.
Hata hivyo Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan akizungumza na vyombo vya habari jana usiku alisema matokeo hayo ni ya awali na kwamba matokeo kamili yangetangazwa na tume yake baada ya kukusanya taarifa kutoka vituo vyote vya kupigia kura.
Wagombea wengine walikuwa wameachwa mbali. Hao ni
Musalia Mudavadi, Peter Kenneth, James Kiyiapi, Martha Karua, Mohamed
Dida na Paul Muite.
Waliokufa wafikia 22
Wapema watu 22 wakiwamo askari polisi tisa waliripotiwa kuuwawa baada ya kuvamiwa na kikundi cha watu zaidi ya 200 huko Mombasa na Kilifi saa chache kabla ya Wakenya kuanza kupiga kura jana.
Saa chache kabla ya uchaguzi huo, askari polisi tisa waliuawa katika mashambulizi yaliyotokea kwenye miji ya Mombasa, Kilifi na Kwale na kuacha wavamizi wapatao 10 na raia wa kawaida watatu pia wakifariki.
Baada ya vifo hivyo, serikali ilipeleka vikosi vya
askari kutoka Mariakani Barracks kwenda kutuliza ghasia hizo wakati
kundi lingine la askari lilitoka Nyali Barracks kwa ajili ya kuweka
doria katika miji ya Mombasa na North Coast.
Taarifa zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa
kwenye mji wa Mombasa askari polisi wanne waliuawa na watu zaidi ya 100
waliovamia kituo cha kura cha Miritini.
Polisi pia ilithibitisha kuuawa kwa watu saba katika mapigano hayo huku na wengine kadhaa kutiwa nguvuni.
Wavamizi wengine waliuawa katika miji ya Kisauni na Kilifi huku polisi wanne wakiuawa Chumani na mmoja huko Chonyi huku watu watatu wakiuawa kwa kupigwa risasi.
Wakati huo huo, mwanamke mmoja wa miaka 72 alianguka na kufariki
akiwa kwenye foleni ya kupiga kura katika kituo cha Kaunti ya Murang’a.
Marehemu aliyefahamuika kwa jina la Wanjiku Maina
alianguka saa tatu asubuhi katika kituo hicho kilichopo Shule ya Msingi
Kaganda katika jimbo la Kiharu na alifariki wakati akikimbizwa Hospitali
ya Muriranjas.
Mkuu wa Polisi Kenya, David Kimaiyo alisema
Kikundi cha Mombasa Republican Council (MRC), ndicho kinachohusika na
shambulio hilo na wafuasi wake wawili wametiwa mbaroni.
“Askari wameelekezwa kutumia silaha kadiri
wanavyotakiwa na sheria, ili kuhakikisha hakuna mauaji mengine ya polisi
na raia yanatokea,” alisema Kimaiyo.
Wajitokeza kwa wingi
Wananchi walijitokeza kwa wingi katika maeneo mbalimbali jana kupiga kura.
Wananchi walijitokeza kwa wingi katika maeneo mbalimbali jana kupiga kura.
Wakati vituo vilikuwa vinafunguliwa saa 12
asubuhi, watu walianza kufurika vituoni saa 8.00 na saa 9.00 usiku ili
kuwahi nafasi na ilipofika muda uliopangwa, misururu ilikuwa mirefu
kupindukia.
Katika vituo, ambavyo Mwananchi ilitembelea, pamoja na wingi wa watu, bado wapigakura walikuwa na matumaini ya kuchagua viongozi wao.
Hata hivyo, kulikuwa na matukio kadhaa ya
kukatisha tamaa, ikiwamo kukwama kwa mashine za digitali za kutambua
alama za vidole za waliojiandikisha (biometric machines).
Baadhi ya mashine, ziliathiriwa na hitilafu wakati
nyingine zikikosa umeme katika vituo vingi vya maeneo mbalimbali ya
Kenya, hivyo makarani kulazimika kutumia daftari la wapigakura.
Mwenyekiti wa IEBC, Hassan alikiri kuwapo kwa hali hiyo na kusema ingetafutiwa ufumbuzi na kuahidi kuwa muda ambao ungepotea ungefidiwa baadaye jioni.
Katika hatua nyingine; watu wawili akiwamo
mwanamke mwenye umri wa miaka 72, walianguka na kufariki dunia wakati
wakisubiri kupiga kura.
Mwanamke huyo alipoteza maisha saa 5.08 asubuhi
katika Kituo cha Kihalu kwenye Shule ya Msingi Kaganda, Kaunti ya
Muranga. Mpigakura mwingine alianguka saa nne asubuhi katika Kituo cha
St Mathew, eneo la Hardy, Nairobi. Alifariki akiwa hospitalini.
Kura Arusha, Dar
Mamia ya wananchi wa Kenya wanaoishi Tanzania walipiga kura katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha.
Kura Arusha, Dar
Mamia ya wananchi wa Kenya wanaoishi Tanzania walipiga kura katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha.
Wakenya hao walipata fursa kwa mujibu wa Katiba Mpya ya nchi hiyo iliyoanza kufanya kazi mwaka 2010.
Ofisa wa IEBC, David Maina ambaye alikuwa
anasimamia upigaji huo Arusha, alisema kwamba hadi kufikia saa tisa
alasiri jana watu 145 kati ya 200 waliojiandikisha, walipiga kura.
No comments:
Post a Comment