Manchester United ambao ni mabingwa wa ligi hiyo msimu huu, Hii leo walikuwa wageni wa Arsenal kwenye uwanja wa Emirates Kaskazini mwa london,
Theo
Walcot alianza kuifungia Arsenal bao la mapema kabisa dakika ya pili ya
mchezo huo ambao BBC ulimwengu wa soka ilikuwa ikuutangaza moja kwa
moja.
United walio chini ya Sir Alex Ferguson
walionekana kutokuwa kwenye kiwango chao kama mabingwa baada ya kuanza
mchezo huo kwa kufanya makosa mengi, na kujikuta wakipewa kadi nne za
njano ndani ya dakika 30 za mchezo huo.
Lakini makosa ya safu ya ulinzi wa Arsenal, hasa
lile la beki Bakar Sagna la kurudisha mpira kwa kipa wake yaani back
pass yaliifanya United isawazishe bao lao kwa njia ya penati baada ya
Sagna kutaka kufuta makosa kwa kumchezea vibaya Robin Van Persie ambaye
aliifunga timu yake ya zamani bila ya kushangilia.
Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kugawana
pointi na Arsenal kufikisha pointi 64 pointi mbili zaidi ya wapinzani
wao Tottenham ambao walitoka sare pia hapo jana na Wigan.
Kwingineko Mashariki mwa jiji la London kulikuwa na michezo miwili kwenye viwanja tofauti,
Chelsea wakiwa wenyeji wa Swansea kwenye uwanja
wa Stamford Bridge, Mchezo uliomalizika kwa vijana wa Roman Abromavich
kuibuka na ushindi wa 2-0, Mabao yao yakifungwa na Mbrazil Oscar Dos
Santos Junior huku Frank Lampard akifunga kwa mkwaju wa penati.
Na Mchezo wa awali kabisa ulichezwa kwenye
uwanja wa Roftus Road kwa QPR kupambana na Wigan, Mchezo ambao
ulimalizika kwa sare bila kufungana.
Matokeo hayo ya sare kwa QPR na Wigan yalizifanya timu zote mbili kushuka daraja la ligi kuu.
Mechi nyingine itapigwa hapo kesho kati ya Aston
Villa na Sunderland, Mechi ambayo itakuwa ni ya kukata na shoka kwani
timu zote mbili zinajitutumua kutoshuka daraja.
No comments:
Post a Comment