Risasi zinarindima! Ni baada ya raia mmoja kupewa kichapo hadi kufariki.
Updates zitafuata
- Gari la Polisi (Difenda) limevunjwa vioo na wananchi wenye hasira kali
- Polisi wameelemewa, wameongeza nguvu ya gari la washawasha
By MTAZAMO
Wanabodi,
Nimepata taarifa ya vurugu huko Kawe na wananchi kuzingira kituo cha
polisi! nimechungulia humu sijaona post juu ya hili nikaona nitoe
taarifa ili wenye taarifa kamili watujulishe maana chanzo changu
hakikuwa na taarifa za uhakika wa chanzo cha vurumai hizo!!
Inasemekana mwanajeshi alikodi bajaji aliposhuka hakuona simu yake
akatuhumu kuiacha kwenye ile bajaji hivyo yule askari akaita wanajeshi
wenzake na kuanza kupiga madereva wa bajaji hadi dereva mmoja
akapoteza maisha.
By platozoom
Ndiyo nami niko Mbezi kuna mabomu ya machzi na risasi zinasikika.
Chanzo ni wananchi kadhaa jana wakiwa kwenye kikao cha kilevi
kutofautiana na Mwanajeshi mmoja na kuzuka vurugu ndogo. Leo wanajeshi
wamepita mtaani kuwatafuta wabaya wao, Wananchi walipowaona wakaanza
kukimbia, kando walimkuta kijana dereva wa bajaji, mmoja wa askari
akaaanza kumpa kipigo (kimsingi hakuwamo kwenye ugomvi) na kupoteza
maisha.
Baada ya hilo Wanachi wakamkimbiza yule mwanajeshii mpaka kwake na kumkabidhi Polisi. Lakini wakati wa sekeseke
la msiba Raia wakasema haiwezekani atuulie Kijana mwenzetu. Wakaandamana hadi kituoni ili kumchomoa mbaya wao.
Na hali ya mambo ndiyo ikawa hivyo.
CHANZO JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment