EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, April 29, 2013

MASTAA WA KIBONGO BANA… WAMEVISHWA PETE ZA UCHUMBA, NDOA ZIMEISHIA NDOTONI.

KATIKA ulimwengu huu kuna mambo mengi yanayofurahisha. Yapo pia yanayosikitisha na utapeli katika uhusiano wa kimapenzi umetamalaki.
Nimeanza na utangulizi huo nikiwa na maana kuwa katika jamii inayotuzunguka inabidi mtu uwe makini lasivyo utajikuta kwenye wakati mgumu hasa kwa wasichana wanaohitaji kuolewa.   

                            Wema Sepetu akiwa na pete aliyovishwa na Dimaond.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuwarubuni wanawake wakiwadanganya kuwa watawaoa, ahadi ambazo hazitimii kwani mapenzi yao huwa yanaishia njiani kabla hawajatimiza lengo na kuwaacha wenzao katika maumivu makali.
 
 Katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, ishu hiyo ndipo nyumbani kwao ambapo leo katika makala haya tutaona orodha ya wasanii ambao wamevishwa pete za uchumba lakini suala la ndoa limeishia ndotoni. Ni kama wanaota lakini wakiamka hujikuta wakijuta kuwa walikosea wapi. Kinachoonekana kwa sasa ni kwamba pete ya uchumba ni ndoano ya kumnasa mwanamke na baada ya kukidhi matwakwa humwacha bila kutimiza ahadi ya ndoa.

                                  H-Baba akimvisha pete ya uchumba Flora Mvungi.

FLORA FESTO MVUNGI
Ni mwigizaji wa filamu za Kibongo anayeishi kinyumba na mwanamuzki wa Kizazi Kipya, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba’.
 

Tangu Flora avishwe pete ya uchumba na H. Baba pamoja na kutolewa mahari, siku zimesonga bila kuona suala la ndoa likiendelea.
Wasanii hawa kila wakiulizwa kuhusu suala la ndoa huwa wanajibu hivi karibuni ambapo kwa sasa kuna madai kuwa tayari Flora ana ‘kibendi’.

ROSE DONATUS NDAUKA
Ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo ambaye alichumbiwa kwa muda mrefu na jamaa aliyekuwa mmoja wa kundi la kitambo la Bongo Fleva kutoka Tanga la TNG, Malick Bandawe.
Rose amekuwa akiahidi kila kukicha kuwa harusi yake iko mbioni lakini umepita muda mrefu hakuna ndoa wala nini na badala yake wamebaki kuishi pamoja kama mume na mke.

OTILIA BONIFACE
Ni mkata mayenu kiraka wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’. Alivishwa pete ya uchumba miaka miwili iliyopita na mume wa mtu anayejulikana kwa jina moja la Ally lakini mpaka sasa ndoa imebaki ndotoni.
Otilia na mchumba wake huyo wanaishi pamoja kama mume na mke na suala la ndoa bado wanajiandaa.

SUZAN CHUBWA ‘QUEEN SUZY’
Ni mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’. Alivishwa pete ya uchumba zaidi ya miaka miwili iliyopita na aliyekuwa rapa wa bendi hiyo, Aimerichard Mwamba ‘G-Seven’ ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake Nairobi, Kenya na kumwacha Suzy Bongo.
G-Seven alimposa Suzy pamoja na kumvisha pete ambapo uchumba wao ulidumu kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni bishosti huyo kuweka wazi kuwa ameamua kuachana naye kwa sababu aligundua kuwa siyo mwaminifu.

ISABELA MPANDA
Ni Miss Ruvuma 2006. Anasaka mkate wa siku kupitia filamu na muziki wa Bongo Fleva. Alivishwa pete ya uchumba kitambo na kutolewa mahari na mwanaume jina kapuni lakini aliishia kupewa mimba na kuzaa.
Baada ya kuzaa Isabela mpaka sasa hajaolewa na amejaliwa kuwa na watoto wawili kila mmoja na baba yake huku ikifahamika kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Luteni Kalama.

MIRIAMU GERALD
Ni Miss Tanzania 2009 aliyevishwa pete ya uchumba na msanii wa filamu za Kibongo, Kennedy Victor ‘Kenny’. Walipanga kufunga pingu za maisha mwezi Juni, mwaka jana lakini hadi unaposoma hapa hakuna chochote zaidi kujaliwa mtoto mmoja wa kiume.

WEMA SEPETU
Ni mwanadada mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo. alivishwa pete ya uchumba na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mapenzi yao hayakufika mbali, waliishia kuachana na mambo ya ndoa yakaishia hapo huku bidada akiendelea kujikusanyia pete za uchumba kabatini kwake baada ya ile ya Yusuf Jumbe.

SHAMSA FORD
Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye kwa muda mrefu amechumbiwa na jamaa mmoja aitwaye Dick. Uchumba wao una zaidi ya miaka miwili lakini ndoa imekuwa ni kitendawili huku wakijaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry.

SALMA JABU ‘NISHA’
Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye aliwahi kudaiwa kuvishwa pete ya uchumba na mwigizaji mwenzake aitwaye Godfrey Kusila kabla ya uchumba kuvunjika na penzi kuhamia kwa mwanamuziki Elibariki Emmanuel ‘Ney wa Mitego’. Hata hivyo, kwa Ney wa Mitego napo uchumba uliota mbawa pamoja na kuwa na mbwembwe nyingi.

                    CHANZO CHA HABARI HII NI GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate