Ngoma inaonekana kuwa bado ni nzito kuhusiana na mirathi ya marehemu
Steven Kanumba kwani taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza
kuwa, hakuna kitu kilichofanyika mpaka sasa kutokana na mvutano
uliokuwepo ndani ya familia.
Akizungumza
na Risasi Jumatano hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora
Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu,
mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka
umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema,
alisikia mzee huyo alituma wawakilishi wake walishughulikie suala hilo
lakini wakachemsha kutokana na kukosa viambatanisho muhimu.
“Mimi
niliamua kusubiri upande wa baba Kanumba wafungue mirathi kwa sababu
Kanumba hakuwa na mtoto kusema nina ulazima wa kuharakisha ili apate
haki zake, cha ajabu hakuna kilichofanyika mpaka sasa,” alisema mama
Kanumba.
Akasema,
kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia
suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili
kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
Credit:Global Pubishers.

kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.Credit:Global Pubishers.
No comments:
Post a Comment