Mpaka sasa watu watatu wameshakufa kutokana na mashambulio ya mabomu
mawili yaliyoripuka wakati wa mbio ndefu za marathon katika mji wa
Boston nchini Marekani
Mabomu mawili yaliripuka kwenye mitaa iliyokuwa imejaa watu karibu na
sehemu ya kumalizia mbio za marathon. Watu wasiopungua watatu wamekufa
kutokana na miripuko ya mabomu hayo yaliyoutikisa mji wa Boston katika
jimbo la Marekani la Massachusettes.
Jee ni magaidi tena?
Watu wengine zaidi ya140 walijeruhiwa katika kadhia ya
umwagikaji wa damu. Vioo vilivunjika na sehemu za miili ya binadamu
ilitapakaa- hali iliyosababisha wasiwasi kwamba magaidi wameishambulia
tena Marekani. Msemaji wa Ikulu ya Marekani ambae hakutaka kutajwa kwa
sababu uchunguzi bado unaendelea, ameeleza kuwa mashambulio hayo
yanazingatiwa kuwa ni kazi ya magaidi.
Akitoa tamko juu ya mashambulio hayo Rais Obama aliepuka kutumia neno
gaidi, alieleza kwamba maafisa wa Marekani hawajui ni nani aliyeyatega
mabomu hayo na kwa nini. Hata hivyo afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani
alisema baadae kuwa miripuko hiyo iliyotokea kwenye mbio za marathoni
zenye jadi ya miaka mingi, inazingatiwa kuwa kitendo cha ugaidi.
Obama asema aliefanya mashambulio atapatikana:
Rais Obama alilihutubia taifa kwa kuwahakikishia Wamarekani kwamba,
tukio hilo litachunguzwa kwa undani. Obama alisema "Tutabainisha nani
ameyafanya mashambulio haya na kwa sababu gani." Ameeleza kuwa wote wale
waliohusika, au kikundi chochote- kitauona mkono mkali wa sheria. Rais
Obama amesema Marekani itamjua alieyafanya mashambulio hayo.
Mabomu hayo mawili yalipishana kwa muda wa sekunde chache tu. Mwokoaji
anaetoa huduma ya kwanza, amesema wanajaribu kupata damu kwa haraka.
Amearifu kuwa wapo waliojeruhiwa kwa kukatika viungo vya mwili na,
wengine waliumizwa na vipande vya vioo, na pote palisambaa damu.
Kutokana na hali hiyo ilibainika wazi kuwa shambulio la kigaidi
limefanyika muda mfupi baadae polisi waliyagundua mabomu mengine mawili
ambayo yalikuwa bado hayaripuka. Mamia ya watu walikuwa wamejipanga
barabarani kushuhudia hatua za mwisho za mbio maarufu za marathon
zinazofanyika katika mji wa Boston kila mwaka. Wakimbijaji karibu alfu
23 walikuwa wanashiriki katika mbio hizo na mara tu, walisikia miripuko
mikubwa miwili na waliona moshi mkubwa na vipande vya vioo - watu wote
waliwambwa na kiherehere.
Ujerumani yasikitishwa
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amesema
ameshtushwa sana na miripuko hiyo na athari zake. "Tunawapa pole jamaa,
familia na marafiki wa wahanga na tunawatakia afueni ya haraka wote
waliojeruhiwa. Tukio la michezo ambalo kwa kawaida lilitakiwa kujaa
utamaduni na furaha tele kwa maelfu ya wakimbiaji na mamia ya maelefu ya
watazamaji kutoka Boston na ulimwenguni kote, sasa limegeuka kuwa
mkosi." Westerwelle aidha amesema angependa kuona uchunguzi unafanyika
haraka na waliohusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle
Mtoto pia afariki
Kwa mujibu wa taarifa za polisi mtoto aliekuwa na umri wa miaka minane
alikuwa miongoni mwa waliokufa. Wahudumu wa hospitali wamearifu kwamba
watu 144 walijeruhiwa 17 miongoni mwao vibaya sana.
Habari zaidi zinasema, kilometa chache kutoka kwenye sehemu ya kumalizia
mbio za marathoni, pana maktaba inayoitwa "JF. Kennedy" iliyowaka moto.
Lakini kamishna wa polisi ya Boston amesema huenda moto huo
ulisababishwa na kifaa cha kulipuka n ahaikubainika wazi kama mkasa huo
unahusiani na mashambulio ya mabomu.
No comments:
Post a Comment