MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sara Kaisi ‘Shaa’
amejinasibu kuwa kiwango alichonacho sasa hakina tofauti na wasanii
wengine wakali kama Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Nassib Abdul
‘Diamond’.
Shaa akifanya vitu vyake.
Shaa aliyabainisha hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifanya
mahojiano na mwandishi wa habari hii aliyekuwa akitaka kufahamu kiwango
cha fedha anachokipata katika shoo zake mbalimbali anazofanya.
“Hivi sasa kama mtu anaweza kumchukua Ommy ama Diamond kwa dau hilo
analowapa, basi anaweza pia kunichukua mimi kwa shoo zake kwa kiwango
cha nyota hao wawili, kwani uwezo ninao,” alisema.
Aliongeza kuwa ili kudumu katika fani ya muziki wa kizazi kipya,
kunatakiwa kuongeza ubora wa kazi kwa kufanya kazi na wadau mbalimbali
wa muziki wa ndani na nje ya nchi.
Shaa alisema kwa sasa wimbo wake wa ‘Lover Lover’ unaendelea kufanya
vema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na Afrika Kusini,
ambako video ya wimbo huo inachezwa zaidi.
No comments:
Post a Comment