Askofu wa kituo cha
maombezi na uponaji cha Overcomers Power Center (OPC) Dkt Boaz Sollo
(kushoto) akimakabidhi tuzo ya heshima mfano wa ramani ya Tanzania
waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa jana katika hafla ya kuchangia
ujenzi wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio Overcomers Fm ,katika
harambee hiyo Lowassa aliahidi kuachangia milioni 15 na kufanikisha
kupata Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo fedha taslimu na ahadi .
Waziri mkuu wa zamani
Edward Lowassa akionyesha tuzo ya heshima mfano wa ramani ya
Tanzania aliyotunukiwa, kushoto kwake ni Askofu wa kituo cha
maombezi na uponaji cha Overcomers Power Center (OPC) Dkt Boaz Sollo
Mheshimiwa Lowassa Alikabidhiwa Tuzo Hiyo katika hafla ya kuchangia
ujenzi wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio Overcomers Fm ,katika
harambee hiyo Lowassa aliahidi kuachangia milioni 15 nakufanikisha
kupata Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo fedha taslimu na ahadi .
WAZIRI mkuu mstaafu Edward Lowassa
amesema kuwa mbali ya kuwa yeye si tajiri ila bado ataendelea
kufanya kazi yake kwa ukaribu zaidi na jamii ikiwa ni pamoja na
kushirikiana na marafiki zake kusaidia na kuwataka wale wote wenye
kusema dhidi yake kuendelea kusema ila hatarudi nyuma katika kutoa
misaada kama njia ya kutafuta baraka za Mungu.
Lowassa ambae pia alikabidhiwa tuzo
ya heshima kwa ajili ya kuendeleza kulipigania Taifa la Tanzania
,huku mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh milioni 15 na mbunge wa jimbo
la Ludewa Deo Filikunjombe akichangia milioni 9 kati ya fedha
zote zaidi ya Tsh milioni 75 zilizochangwa kwa ajili ya kuendeleza
ujenzi wa kanisa la OPC mkoani Iringa kama njia ya kuhamasisha amani
katika Taifa ametaka watanzania kuwapuuza wale wote wanaoeneza
siasa za uchochezi .
“Nataka kuwaomba leo wachukieni
wachochezi na pia niwaelezeni kuwa mimi si tajiri ila nina utajiri
wa watu na ushawishi na ninafanya mambo haya ili kumbukumbu yangu
iweze kuandikwa Mbinguni na nimekuwa nikialika watu wengi na
nimekuwa nikifika wacha wenye kusema waseme watasema ila usiku
watalala wenyewe ….sitaacha kusaidia kwa kuogopa kusemwa”
Akizungumza katika hafla hiyo
iliyoandaliwa na kituo cha maombezi na uponyaji mkoani Iringa
Overcomers Power Center (OPC) na kufanyika katika ukumbi wa St
Dominic mjini Iringa leo Lowassa alisema kuwa yeye si tajiri kama
ambavyo watu wanavyofikiri ila amekuwa akipewa nguvu na rafiki zake
ambao wamekuwa wakimuunga mkono pindi anapoalikwa katika hafla mbali
mbali.
“Nataka kwanza kuwashukuru ndugu
zangu wa mkoa wa Iringa na napenda kumshukuru zaidi Askofu Dkt Boaz
Sollo kwa kunialika mkoani Iringa …..ila napenda kuwaeleza kuwa si
kwamba nachangia michango mbali mbali katika jamii kama mimi ni tajiri
ila mimi ni mtumishi nisiye na faida na nayaweza yote katika yeye
anitiaye nguvu Pia nawashukuru sana wabunge wenzangu ambao
wamepata kushiriki name leo katika ziara hiyo akiwemo mbunge
machachari bungeni Deo Filikunjombe , Kagi Lugola na dada yangu
Ritta Kabati bila kumsahau mbunge Mendradi Kigola kwa kuungana nami leo
naamini nao wamepanda mbegu bora”.
Lowassa alisema kuwa anatambua bado ana
mialiko migi sana na lazima anaifanyia kazi mialiko yote kama ambavyo
jamii imepata kumwalika na kuwa hata hatua ya mkoa wa Iringa kumpa
tuzo hainamanishi kuwa ni mwisho wa yeye kualikwa.
Hata hivyo Lowassa alisema kuwa kwa
upande wake anapongeza jitihada za askofu Dkt Sollo kwa kuwa na
mipango na mitazamo ya kulisaidia Taifa kwa kuanzisha ujenzi wa
kanisa kwa ajili ya kudumisha amani na kwenda mbali zaidi kwa
kuanzisha kituo cha radio Overcomers Fm chambo ambacho
kitatumika kudumisha amani ya mkoa wa Iringa na Taifa pia
Kuhusu amani ya Taifa la Tanzania
LOwassa alisema kuwa alikuwa ni miongoni mwa watu walioalikwa Kenya
katika sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ila
sehemu kubwa ya wote waliotoa salam zao walitumia muda mwingi
kupongeza vyombo vya habari kwa kulinda amani na hivyo kuvitaka
vyombo vya habari za Tanzania na wanahabari kuendelea kuandika habari
bila kuhatarisha amani ya Taifa
“Tusiruhusi amani ya nchi yetu
iyumbishwe na mtu awaye yeyote na kila mtanzania anapaswa kulinda
amani hii kwa nguvu zote ….Nawaombeni wanahabari tunzeni amani
yetu…wapuuzeni wale wote wanaoch0chea machafuko katika Taifa hili
….tuachane na udini wala ukabila katika taifa letu ila “
Katika hatua nyingine Lowassa
aliwapongeza wabunge wa CCM ambao wameendelea kupigania wanyonge
bungeni akiwemo Deo Filikunjombe mbunge wa Ludewa na mbunge wa jimbo la
Mwibara Kagi Lugola kuwa ni miongoni mwa wabunge ambao amekuwa
akiwapenda kutokana na kusema kweli bungeni.
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe
alisema kuwa mbali ya kutoa ahadi ya kuchangia kiasi cha Tsh milioni 9
ila bado atamwalika Lowassa jimboni kwake Ludewa na kuwa kanisa
hilo la OPC halijakosea kumpa tuzo ambayo ni ramani ya Tanzania
kutokana na Lowassa kuwa ni mtu wa watu mpendwa na watu na kuwa tuzo
hiyo ina maana kubwa na hawajakupa ramani ya jimboni kwako Monduli
Filikunjombe alimtaka Lowassa
kuendelea kuchapa kazi na kuwa hajakosea kuwaalika wao kwani
bungeni kuna wabunge zaidi ya 300 ina amewachagua wao pekee ni
jambo la kumshukuru na kumfananisha L0wassa na mti unaopigwa mawe
kuwa ni mti wenye matunda
“Nakuomba Lowassa simama Imara sisi
wana Iringa tupo nyuma yako na niseme tuna kazi kubwa ya kuifanya
katika Taifa hili kubwa ni kumwomba Mungu na makanisa na dini zote
kuungana katika maombi zaidi kwani vita ni kubwa mbele “
Kwa upande askofu Dkt Sollo mbali
ya kumpongeza Lowassa bado alisema kuwa wao kama kanisa wataendelea
kumwombea afya njema na kuona kuwa mambo yake yanafanikiwa na ndio
maana ya kumpa tuzo hiyo ya heshima.
Sollo alisema kuwa mchango wa TSh
milioni 15 ulioahidiwa na Lowassa na ule wa milioni 9 ulioahidiwa na
mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ni mchango ambao wao
wanaupongeza na kuwapongeza wabunge wengine akiwemo Ritta Kabati
aliyeahidi Tsh milioni 2 ,Benki ya wananchi Mufindi milioni 2 ,
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu milioni 2
mfanyabiashara Salim Abri milioni 1 na wengine wengi ambao
wamepelekea kupata zaidi ya Tsh milioni zaidi ya 75 pesa taslim na
ahadi .
No comments:
Post a Comment