EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, May 5, 2013

AZAM YATOLEWA KWENYE MASHINDANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA BAADA YA KUFUNGWA 2-1 NA AS FAR RABAT.

TIMU ya Azam FC siku ya jana imefungwa mabao 2-1 AS FAR Rabat kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani mchezo uliochezwa Uwanja wa Prince Moulay Abdellah nchini Morocco

Azam ilihitaji sare yoyote ya mabao ili iweze kufuzu lakini dakika ya 81 ilipata penalti ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini fundi wa upigaji wa michomo hiyo, John Raphael Bocco alikwenda kugongesha mwamba mpira huo na kurudi uwanjani.

Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita, mfungaji John Raphael Bocco kwa mpira wa adhabu, baada ya beki mmoja wa AS FAR Rabat kushika mpira kwenye eneo la hatari.

Iliwachukua dakika sita tu AS FAR Rabat kusawazisha kupitia kwa Abdelrahim Achchakir kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki David Mwantika kumchezea rafu mchezaji wa AS FAR Rabat.

Abdelrahim Achchakir alitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Brian Umony dakika ya 35 lakini SA FAR Rabat wakiwa pungufu waliongeza bao la pili kupitia kwa Mustafa Allaoui alipiga vizuri shuti la mpira wa adhabu dakika ya 42.

Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kuwa wa kasi na  kushambuliana kwa zamu na dakika ya 56 beki wa Azam David Mwantika kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mchezaji wa AS FAR Rabat. Na Waziri Salum alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 75 baada ya kumchezea rafu Kaddioiu Yuossef.

Pamoja na Azam kuwa pungufu waliendelea kulishambulia lango la AS FAR Rabat na dakika ya 81 beki wa AS FAR Rabat alishika mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi akamuru penalti ambayo Bocco alikosa baada ya shuti lake kugonga mwamba.

Azam imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya mchezo wa awali wiki mbili zilizopita kutoka sare ya bila kufungana Dar es Salaam na Waarabu hao.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Gaudence Mwaikimba dk79  na Brian Umony/Khamis Mcha dk70.

AS FAR Rabat; Ali Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal Salaheddine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui, El Kodry Yassine, El Bakkali Medamine na El Yousfi Mostafa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate