SERIKALI imekanusha taarifa zinazoeleza kuwa Tanzania inaongoza kwa vitendo vya rushwa na urasimu barabarani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu, Mkiwa Kimwanga (CUF).
Katika swali hilo, mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itaondoa
vitendo vya urasimu na rushwa vilivyokithiti nchini na kuifanya
Tanzania kuongoza.
Akiendelea kujibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alisema si kweli
kwamba Tanzania inaongoza kwa vitendo hivyo, kwani rushwa ni tabia ya
mtu.
Katika swali la msingi, mbunge huyo alihoji hatua zinazochukuliwa na
serikali katika kuondoa adha ya urasimu unaolalamikiwa na wadau wa
usafirishaji na wafanyabiashara nchi jirani wanaotumia Bandari ya Dar es
Salaam.
“Kwa muda mrefu sasa wadau wa usafirishaji na wafanyabiashara wa nchi
jirani wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam wamekuwa wakilalamikia
urasimu uliopo barabarani unatokana na vituo vingi vya mizani, TRA na
kusimamishwa mara kadhaa na askari wa usalama barabarani, jambo
linalowafanya kuchelewa bandarini na ama kuharibika kwa bidhaa
walizobeba,” alisema mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri alisema kulingana na sheria ya
Usalama Barabarani ya mwaka 2001 magari yote yenye uzito kuanzia tani
3.5 na kuendelea yanatakiwa kuingia kwenye vituo vya mizani na kupima
uzito wakati wa safari zao.
Alisema lengo kuu la kupima magari ni kulinda barabara na madaraja ambayo ujenzi wake unagharimu taifa fedha nyingi sana.
Aidha alisema Tanzania kuna vituo saba vya mizani kwenda Kisumo na si
30 kama alivyosema mbunge na kuongeza kuwa hivyo vingine havijui.
“Katika kuboresha shughuli zinazofanywa katika vituo hivyo vya mizani,
serikali imejipanga kununua mizani ya kisasa, ili kuboresha utendaji
kazi na kuifanya kazi hiyo kuwa rahisi,” alisema Lwenge.
No comments:
Post a Comment