WASANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
na Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ wamemaliza bifu lao lililokuwa
likifukuta kama moto wa kifuu mwishoni mwa wiki mbili zilizopita.
Akizungumza na mwandishi wetu katikati ya wiki hii, Baby alisema
alikuwa Mkoani Geita kwa ziara ya kikazi lakini alipigiwa simu na Wolper
akimuomba msamaha kutokana na tofauti zao zilizosababishwa na nyumba ya
kupanga.
“Nimeona bora yaishe kwa sababu Wolper amekubali kosa na
mimi siwezi kuendeleza bifu lakini kama asingeniomba msamaha
tungefikishana mbali,’’ alisema Baby Madaha na kuongeza:
“Nimemalizana na Wolper ila kesi itabaki kwa mwenye nyumba,
nitapambana naye hadi atakaporejesha mkwanja wangu japokuwa nimepata
nyumba nyingine maeneo ya Mikocheni.”
Wolper na Madaha waliingia
kwenye bifu zito baada ya Madaha kukuta nyumba aliyoilipia shilingi
milioni 3.6 kama kodi maeneo ya Kinondoni jijini Dar imechukuliwa na
Wolper kabla yeye hajahamia.
No comments:
Post a Comment