EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 9, 2013

Elimu ndiyo kikwazo kwa uigizaji Tanzania.

Napenda uigizaji.
Nilikuwa mwigizaji nikiwa shule lakini nikaachia huko huko kwani enzi zetu mambo ya kuigiza hata katika redio wakati huo tulikuwa tunaona ni kazi ya watu wasio na elimu kubwa. Naamini tumeendelea hivyo mpaka sasa.

Watu wengine wanasomea masuala ya sanaa mpaka ngazi za juu za shahada ya kwanza hata zile za mizania lakini sijui ni wangapi wameamua kutumia elimu yao katika fani hii ya uigizaji.
Mapenzi yangu ya fani ya uigizaji yananifanya niangalie sana filamu, vichekesho na maigizo mengine ya nchi nyingi ulimwenguni kupitia televisheni, ‘DVD’, Mitandao n.k. Nalinganisha uigizaji wetu na wa wenzetu naona bado tuko nyuma.

Ni ukweli uwezo wetu kifedha bado ni mdogo na najua kutengeneza filamu moja inahitaji fedha nyingi, lakini bado hata kile kidogo tunachokitengeneza ni hafifu.
Hadithi zinazofanana, vipengele (scenes) visivyo na ujumbe wowote, n.k. vyote hivyo vinaonyesha kwamba safari yetu katika fani hii inayopendwa bado ni ndefu.

Nayasema haya kama mtazamaji wala si mtaalamu wa uigizaji, nikitambua kwamba hahitaji mtu kuwa mpishi mzuri kutambua kwamba chakula kilichopikwa ni kitamu au la. Ndiyo maana katika makala haya nawaalika wataalamu katika fani hii kuingilia kati na kuinusuru.
Lazima nikiri kwamba watu wa nchi hii vipaji vya kuigiza wanavyo, kwani wengi wao wanafanya shughuli hii kwa kupata mafunzo kidogo tu tena kupitia kwa walimu ambao nao hawana utaalamu wa kutosha.

Lazima tutambue kwamba dunia inakuwa kijiji, kwa ving’amuzi, mitandao, n.k watu tunapata fursa ya kuangalia filamu na maagizo mengine kutoka nchi za nje.
Si rahisi mtu aache kuangalia filamu toka nchi nyingine kwa sababu tu ya uzalendo.
Sasa starehe hailetwi na nadharia ya uzalendo bali na kile kinachoburudisha bila kujali kinatoka kona gani ya dunia hii. Hivyo hakuna ujanja katika hili.

Ni lazima waliopo kwenye fani hii watuletee kilicho bora toka kwenye hadithi, uandishi, mpangilio wa vipengele mbalimbali, uigizaji wenyewe na kila kitu kihusucho uigizaji. Hili linahitaji wale waliosomea fani hii hasa wale waliomaliza vyuo vikuu kuingilia kati.
Kuna wakati mwigizaji mmoja alisema kwamba fani hii ina upungufu wa waandishi (script writers) na hiyo ni changamoto kubwa sana kwao.


Hata mimi nakubaliana naye kwamba hii ni changamoto kubwa lakini wataalamu katika uandishi wa uigizaji wanaweza kuikabili. Kuna watu wamemaliza shahada zinazowawezesha kuwa waandishi wazuri tu wa filamu na maagizo mengineyo.

Tunawaomba watu hawa watumike katika kuandaa maandishi. Natambua kwamba itamaanisha gharama zaidi kwa wenye filamu zao, lakini kuna maana gani kuepuka gharama halafu mtu kuleta au kupeleka sokoni kitu ambacho hakina ladha? Hii habari ya ‘stori’ - Bwana X, ‘producer’ Bwana X, ‘script writer’ – Bwana X, ‘Director’ – Bwana X n.k. hazitatufikisha kokote.

Kama wenzetu waliotutangulia wanatambua uwezo wa watu tofauti katika nyanja hizo, kwa nini sisi tuone ni kazi inayoweza kufanywa na mtu yeyote ili mradi tu aweze kuigiza?
Lazima tutambue kwamba uandishi ni taaluma inayohitaji mtu kukaa mafunzoni kwa muda fulani na watu ambao wana elimu na uzoefu mkubwa wa fani hiyo.

Elimu hii ikiongezwa na kipaji mtu katika uandishi kinakuja kutoa mwandishi mzuri ambaye akitutengenezea maandishi ya filamu yatatufanya tupate filamu nzuri sana.
Kama waigizaji wanataka kuandika wenyewe filamu zao basi wakubali pia kuingia shule kwa ajili ya hiyo. Lakini bado watambue kwamba kuna suala la kipaji katika hilo.
Licha ya elimu na kipaji kuna suala la muda. Mtu kujibebesha majukumu mengi kunaweza kumsababishia kutokuwa na ufanisi kwenye majukumu yote aliyojibebesha.

Nakumbuka miaka iliyopita tulikuwa na akina Penina Mhando na wasomi waliobobea waliokuwa wanaandika michezo mbalimbali sasa tunahitaji watu wa aina hiyo wengi zaidi.
Tukiacha suala la uandishi, tunahitaji pia waigizaji wenye uelewa wa juu wa kile wanachokifanya. Mimi hupenda kuangalia ‘Isidingo’ na kitu kimoja kinachonifurahisha katika ‘Isidingo’ ni uigizaji unaoonekana kama ni halisia.

Wa kwetu wanashindwa kuonyesha hisia inayotakiwa, utakuta waigizaji wanawake tena waliobobea katika fani hii wakiwa wanaigiza kulia kwa uchungu na watazamaji tusiione hisia hiyo.
Huu ni udhaifu katika uigizaji. Wale tunaowaona wanaigiza kwa umahiri huo niusemao ni kwamba wanakuwa pia wana elimu ya kiwango kinachoridhisha.
Tuangalie wa kwetu na elimu zao, hakika elimu zao ni za chini na upeo wao mdogo katika fani hii. Wengi wanafikiria kwamba kuigiza hakuhitaji mtu kusoma, na uthibitisho ni wale wanaoacha shule wakikimbilia kwenye uigizaji kwani kwa mawazo yao kwamba katika kuigiza kunawezekana hata kama huna elimu. Huko ni kujidanganya.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate